KERO Kelele usiku kucha Mtaa wa Alesika, Mbezi Beach kutoka Amigos Pub na Kanisa la Angels Ministry ni kero kubwa, tumechoka!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi wakazi wa Mbezi Beach kwa Komba mtaa wa Alesika Road jirani na Ofisi za Airtel tunateseka kwa kulazimika kukesha pamoja na waumini wa kanisa la Angels Ministry ambao wapo kushoto kwetu na Amigos Pub ambayo ipo kulia kwetu. Wanakesha kwa makelele usiku kucha na kuondoka saa 11 asubuhi.

Kwa upande wa Kanisa wamekuwa wakifanya hivyo Mara kwa Mara na kwa upande wa Amigos Pub wamekuwa kila siku wakikesha hadi asubuhi wakilewa na kupiga muziki kwa sauti ya juu na kama haitoshi wanaimba kwa sauti na kusababisha makelele na usumbufu kwa wakazi waliopo jirani ikiwemo wazazi wazee na baadhi ya Familia zenye watoto wenye changamoto ya afya ya akili.

Wahusika hawa walianzisha biashara zao wakati tayari wametukuta katika makazi hayo. Tulishaandika barua hadi ngazi ya wilaya lakini hazikufanyiwa kazi licha ya juhudi za wananchi wa hapa. Zaidi tunaamini wanakula rushwa ndio maana hawafanywi lolote maana nchi hii wameiweka mikononi mwao wala hawajali ukienda kuwasemesha wanakuona kichekesho tu.

Mbona waheshimiwa wenye vyeo serikalini hawakubali makanisa na hizi Pub uchwara maeneo wanamoishi wao? Hatukatai wao kusali lakini waweke 'sound proof '.

Serikali ya Mtaa hadi wilaya imekaa kimya kwa sababu Mkuu wa Mkoa Mh. Albert Chalamila aliwaaminisha kuwa huu ni mji kwa hiyo wasiopenda kelele warudi vijijini.

Hii si sawa kwa sababu walitukuta na pia ni makazi ya watu na tunalipa kodi kama wao tofauti yetu na wao ni kwamba wao wanatoa rushwa. Tunaambiwa tusijichukue hatua mikononi mwetu lakini haya yanafanyika kwa sababu watu tumechoka na yanayoendelea sasa kifuatacho mtaskia mlio tu TUMECHOKA SANA TENA TUMECHOKA HASWAA.

Tunaomba Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuingilia kati na kuchukua hatua juu ya kero hii, Watoto wetu wanapata shida usiku.

Alesika.png
Pia soma
 
Hatukatai kila mtu ana haki ya kuamini chochote anachoamua, lakini imani yake isiwe makwazo kwa sisi wengine mpaka tunashindwa kufanya shughuli zetu. Vile vile mtu kuwa na baa yake ni ajira hizo anatoa kwa watu wengine zinazosaidia kuendesha maisha yao, lakini malele yaliyokithiri hayakubaliki.

Kanisa hili la Kanisa la Angel's Ministry limekuwa likipiga makelele kupitiliza, halina kizuia sauti (sound proof) na hivyo kelele inayopigwa inafika moja kwa moja kwetu. Wanafanya mikesha karibu kila siku usiku wakidai wanatafuta miujiza, jamani kwa makelele yanayopigwa ni changamoto kulala na hata kuconcetrate kufanya majukumu yako.

Sasa kama mimi niko mzima wa afya napata tabu fikiria wazee, wagonjwa, wajawazito na watoto wanaathirika vipi na makelele haya. Karibu na kanisa hili kuna baa ya Amigus Pub ambao wanakesha karibu kila siku wakiimba na ni kwa sauti kubwa yaani kama vile wanashindana na kanisa, sasa ukiwajumlisha wote wawili ni kama tupo Jehanamu ndogo tukisubiri kwenda kusulubiwa na Mungu upande wa pili.

Tumeshalalamika mpaka katika uongozi wa mtaa kufikia hatua ya wao wakaitwa na kuelezwa usumbufu wanaotusababishia lakini hakuna kilichosaidia, ndio kwanza wanatutambia hatuna cha kuwafanya sababu uongozi upo upande wao. Na hilo limethibitika kweli, sababu hakuna kilichofanyika mpaka sasa mwaka umefika, si kwa kuweka soundproof wala kupunguza makelele yao. Hii ni noise pollution, kwanini hawachukuliwi hatua?

Ni mpaka tukatoe rushwa ndio msikilize malalamiko yetu? JamiiForums naomba mtusaidie kufikisha malalamiko yetu, mnaweza mkatuma mtu wenu kuja kuuliza wakazi wa karibu na kanisa hilo mjionee wenyewe jinsi watu wanavyoathirika na hili na kwa namna gani watu wamechoshwa na hali hii.

Wana uhuru wa kuabudu na kuendesha biashara yao ya baa lakini wasifanye kwa namna ambayo inatuumiza wengine, na sisi pia tuna haki ya kuishi katika mazingira mazuri bila usumbufu. Tangazo la Mkuu wa Mkoa Chalamila ndio kama limezidi kuwaongezea kiburi.

Tunaomba mtusaidie jamani, TUMECHOKA, labda ikitokea kwenu mamlaka zitatusikiliza na kufanyia kazi hili.
 
Kwetu pia kuna jamaa eneo lake kakodisha kikanisa flani cha mchongo, sasa hilo eneo lipo juu, huku tulipo kupo kwa chini...daah huo mziki unaotoka kama unapigwa kutokea chumba cha pilii aisee...
 
Poleni sana.

Swali:Eneo ni Skwata?

Yes: Hapo hawana kosa bali ni utashi wao tu unahitajika.
No: Matumizi yake ni Makazi,Biashara,huduma za Jamii?
 
Back
Top Bottom