Samico Tanzania
JF-Expert Member
- Feb 6, 2022
- 414
- 1,043
Kama ilivyo chumvi kwenye mboga, ndivyo ilivyo umhimu wa madalali!
Nilikuwa nawachukia sana madalali hapo mwanzo, lakini baada ya kutuliza kichwa sawasawa hawa jamaa nimegundua kumbe udalali ni nguvu ya kiroho wala siyo Mtu!
Dalali ni roho kamili inaweza kufanikisha jambo lako au kukufelisha vibaya mno na usiamini macho yako.
Ninaposema Dalali ninamaanisha mtu yoyote anaefanikisha jambo au biashara akiwa kama mtu kati!
Huyu mtu kati (dalali) anauwezo wa kumgeuza geuza bosi kuliko ile kawaida, hawa jamaa wana nguvu ya ajabu kuliko kawaida! Kiboko ya dalali ni dalali mwenzie kuliko wewe!
Anauwezo mkubwa sana wa kuharibu biashara ndani ya sekunde moja tu!
Nitawapa mifano hai kabisa ili hili somo mlielewe!
Siku moja nikawa natafta chumba cha kupanga, nikasema wacha nikanyage mguu kwa mguu maana nilikuwa na pesa kamili sikuwa na hela ya ziada kumlipa dalali, nikapita mtaani kuulizia kama kuna chumba cha kupanga!
Kila nyumba niliyopita kwanza nilionekana kama mtu wa ajabu sana, fukara, wengine waliniona kama siko sawa!
Wengine hadi wanauliza kabisa unajishughulisha na kazi gani, nikawajibu mimi ni fundi umeme na ujenzi lakini mwisho wa sikuwakasema hawapangishi fundi duh! (nikasema moyoni hata Yesu alikuwa mtoto wa fundi lakini mbona tunazarauliana hivi ila fresh nikasonga mbele)
Nikaenda nyumba nyingine nikakuta mzee mwenye nyumba naye akasema hapangishi mtu ambae hana ajira serikalini (Nikawaza hivi kumbe tatizo la uelewa ni kubwa namna hii katika jamii yetu)
Baada masaa karibu 7 ya kuzunguka nikaenda kwenye kibanda kula! Hapo ndipo mama ntilie akanambia nenda pale kwenye mti huwa kuna madalali wanakaa kaa hapo kijiweni kawaulizie!
Nikamkuta jamaa mmoja akanambia chumba umepata, tena mwenye nyumba anaroho ya kizungu! Nikamuuliza nyumba iko wapi akanielekeza nyumba ile ile niliyopita nikachomolewa na kuambiwa hawapangishi Fundi!
Nikamwambia dalali hapo hapana nimepita nikaambiwa hawapangishi fundi, dalali akasema hiyo kazi niachie mimi wewe tulia!
Fundi samico nikatulia kimya tukaenda!
Dalali akafika hodii mwenye nyumba akaitika karibu,
Dalali: Ulisema Sikuletei wapangaji sasa andaa mkataba
Mwenye nyumba: Akamjibu tafta wapangaji wa kueleweka unaniletea fundi anisumbue kulipa kodi.
Dalali: Umepita pita mjini huko? Unamjua MFUGALE?(mungu amlaze mahala pema huyu mzee)
Mwenye nyumba: huyu wa wizara ya ujenzi?
Dalali; ewaaaah sasa huyu ni moja ya vijana wake wa kazi! Nimemsubiri tangu asubuhi kumbe alipotea!
Dalali: yaani huyu ni moja ya fundi tegemewa sana bila yeye kazi za wizara zinasimama!
Mwenye nyumba: Kijana karibu sana, nyumba ndiyo hii, unafamilia n..k...story cut....
Tangu kipindi hiko nikajifunza mambo mawili!
1. Tatizo za ajira Tanzania siyo la kiserikali bali ni tatizo la kijamii yaani mifumo ya kijamii au fikra za wanajamii zimefungwa kwenye mfumo wa kutokuishughulisha akili
2. Mfumo automatiki unalazimisha mtu wa kati asimame kama kiunganishi kwasababu jamii inapenda matokeo zaidi kuliko njia za kupata matokeo
Tangu nitambue hili nikasema siku nikupata nafasi ya kuonana na viongozi nitawambia mawazo yangu japo nimeishia la saba wao watayaweka kisomi zaidi!
Kwasasa huwezi kupata bingo la maana bila kuwa na mtu kati!
Hata humu jamii forum kila siku napost namba yangu 0711756341 lakini huwa naitwa sehemu unafanya kazi halafu ukimpa mtu namba anakujibu kumbe namba yako nilikuwa nayo!
Tanzania dalali anasikilizwa zaidi kuliko mtaalamu mimi nawapenda sana madalali! Wanachopanga wao huwa sipingi kabisa!
Popote mlipo madalalj pokeeni maua yenu leteni kazi namba yangu ni ileile fundi samico Tuishi!