Ninataka kazi ambazo ninaweza kuwashauri wadogo zangu au marafiki waliopo Tanzania waweze kuweka malengo yao katika maisha,
Kazi hizo ziwe na uwiano mzuri kati ya kipato na ubora wa maisha yani balance of life, mfano unaweza kukuta Kazi inakulipa million 3 kwa mwezi lakini, nyumbani huonekani, weekend zote karibu upo kazini, yani unazeeka kwa lazma, hapohapo kuna Kazi unalipwa laki 6 kwa mwezi, haina stress una muda mwingi wa kukaa na familia na kufanya mambo yako binafsi kama kilimo au ujasiriamali na watoto wanakuona karibu kila siku ya wiki.
Na kuongeza, isiwe ya kuhamishwa hamishwa hovyo kwenda kuishi sehemu usizozipenda na kukosa base ya familia kama ngedere .