Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,500
- 3,698
Baada ya malalamiko ya muda mrefu ya Wakazi wa Kawe katika Wilaya ya Kinondoni, hatimaye Kituo cha Mafuta cha 'Lake Oil' kilichokuwa kimejengwa karibu kabisa na makazi ya watu kimeanza kubomolewa.
Kituo hicho kilichokuwa karibu pia na stendi ya daladala ya Tanganyika Packers kilikuwa kinahararisha maisha ya watu na kuwapa wasiwasi mkubwa Wakazi wa eneo hilo lakini sasa baada ya kuona kinaanza kubomolewa wanaanza tena kupata amani.
Tunashukuru Mamlaka husika kwa kusikia kilo hiki na tunaamini hali hii ya kujenga vituo vya mafuta kwenye makazi au karibu na makazi ya Watu itakoma kwani haina faida yoyote zaidi ya kuhatarisha maisha.
Kawe: Ubomoaji wa Kituo cha Mafuta cha Lake Oil kilichokuwa karibu na Makazi ya Watu
Hali ilivyokuwa mara ya kwanza kweli ilikuwa ni hatari sana, iwa kungetokea shida yoyote eneo hili basi maafa yake yangekuwa ya kihistoria sana. Wizara ya Ardhi chini ya Jerry Silaa na Mamlaka zote zilizohusika katika kufanikisha hili tunashukuru.
Eneo Kituo hicho kilipojengwa na ukubwa wa athari iwapo kingelipuka
Pia soma:
1. Kuongezeka kwa Ujenzi wa Vituo vya Mafuta kwenye makazi ya watu Serikali inasubiri ya Morogoro yatokee ndio ichukue hatua?
2. Pongezi Waziri Silaa kumsimamisha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi vituo vya Mafuta vinajengwa katikati ya Makazi