Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 226
- 266
Wana JF hebu tujadili hili jambo la kujiandikisha maana naona kama limedoda kupita kiasi maana watu ni kama wamesusa hivi kujiandikisha
Zimebaki siku mbili tuuu kabla ya kufungwa kwa zoezi la uandikishaji kwa wakazi kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mtaa.
Lakini juzi hapa Tabora nilienda kujiandikisha kwenye moja ya kituo.. nilichogundua ni kwamba afisa wa uandikishaji anaweza kukaa mpaka saa nne hajapata mtu wa kumuandika hii inamaanisha nini?
Nilipongea na huyo mhudumu kuhusu hali ya watu kujitokeza kujiandikisha, alisema hali ni mbaya sana kwa siku anaweza kuandikisha watu wawili hadi watatu na tangu aanze uandikishaji hajafikia idadi ya watu 150 jambo ambalo ni hatari..
Nikazunguka tena kituo kingine nikakuta vituo kama nitatu ni vyeupe.. hakuna wanaoenda kujiandikisha kwahivyo zoezi hali ni mbaya sana na watu wamesusa hatari..
Baada ya kuliona hilo nikaenda zangu kwenye kijiwe cha kahawa nikawa nabadilishana mawazo na wenzangu, kuna mzee wa busara mmoja akasema sababu za watu kukosa hamasa ya kujiandikisha ni serikali kuua upinzani wakidhani kwamba wamefanikiwa kumbe hata watu wanachoka kuona wanapelekeshwa..
Zamani Chadema, CCM, CUF, na vyama vingine walikuwa wanahamasisha watu kujiandikisha lakini saivi CCM wao ndio wanaifanya hiyo kazi lakini kwakua mwitikio ni sifuri ndio maana unaona wanacheza rafu za kuandikisha wanafunzi na wale ambao hawajafika muda, watu hawana hata mwamko wowote ndio maana wanachukulia poa.
Sasa iko haja kwa serikali kuepukana na haya mambo ya kuudidimiza upinzani wakidhani wamefaniwa kumbe wanajizika wenyewe.
Kwa ujumla Watu hapa Tabora hawajajiandikisha inavyotakiwa na huenda kwa mkoa mzima wasifike lengo maana watu hawana hata wazo wanamka wanafanya kazi zao hawana muda na kujiandikisha...