Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 18,664
- 47,064
Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, na Wateule wote wa Eais, ni wasaidizi wake Rais.
Hao wateule wa Rais hawakuchaguliwa na wananchi kwenye hizo nafasi zao bali Rais amewateua ili wamsaidie kutimiza majukumu ya Serikali. Ndiyo maana haiwezi kutokea wateule hao wakafanya yaliyo kinyume cha Rais, halafu wakaendelea kuwepo kwenye nafasi zao. Ni kutokana na ukweli huo, ndiyo maana, ndani ya Serikali, huwa KUNA UWAJIBIKAJI WA PAMOJA.
Ndani ya Serikali, ikitokea wewe ni mteule wa Rais, na anayoyataka Rais na baraza zima la Mawaziri, wewe ukawa hukubaliani nayo, unachoweza kukifabya ni kujiuzulu, maana huwezi kubakia ndani ya Serikali halafu ukawa hukubaliani na yale mkuu wa Serikali na Baraza lake la Mawaziri, wanayataka.
Na kwa upande wa Rais, kama mteule wake yeyote akatenda au kunena kinyume na matakwa, dhamira au msimamo wake, lazima atamwondoa huyo mteule wake. Rais akimwondoa mteule wake kwenye nafasi yoyote ile kwa sababu ya kile ambacho umma umeona ni uovu, inakuwa ni ujumbe wa Rais kwa wananchi kuwaambia kuwa huyo mteule wangu alichokitenda au kukinena siyo msimamo wangu na wa Serikali yangu. LAKINI Rais akikaa kimya baada ya malalamiko mengi dhidi ya kauli au vitendo vya mteule wake, huo ni ujumbe tosha kwa wanaolalamika kuwa kilichonenwa au kutendwa na mteule huyo wa Rais ndiyo msimamo wa Rais na Serikali yake nzima.
Hivyo wananchi ni vema tukatambua kuwa kwa kauli ile ya Nape, kuwa kura ya mwananchi kwenye box la kura haina maana yeyote, na kwamba mwenyekiti wa mtaa/kijiji, diwani, mbunge na Rais wanaamliwa na wale wanaohesabu kura, na siyo wapiga kura, kwa vile Rais hajatamka chochote dhidi ya kauli hiyo, na wala hajamchukulia hatua yeyote Waziri Nape, basi ifahamike kuwa huo ndio msimamo wa Rais Samia na Serikali yake nzima.
Hii ina maana kuwa uchaguzi wa mwaka huu na hata wa mwakani, ni maigizo tu kama ilivyokuwa vipindi vilivyopita, na wananchi kwenda kupiga kura ni kupoteza tu muda, kwa sababu watakaohesabu kura, ambao kiuhalisia ni wateule wa Rais, ndio watakaoamua nani awe mwenyekiti wa mtaa/kijiji; nani awe diwani, nani awe mbunge na nani awe Rais. Na jambo hili halishangazi, bali linatoa jibu kwa nini Rais amegoma kabisa nchi kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, badala yake akaamua tu kubadilisha jina la Tume ambayo haipo huru, sasa iitwe tume huru.
Wananchi kama tunajitambua, kwa kuzingatia muundo wa Tume, kauli ya Serikali kupitia Nape, kauli ya Rais Samia akiwa Makamu wa Rais, kauli ya aliyekuwa waziri Anna Tibaijuka aliyesema kuwa alimwambia Lowasa kuwa mfumo wa nchi yetu hauruhusu kuwa na Rais kutoka upinzani, ni aheri wananchi tukaachana na kupoteza muda kwenye chaguzi hewa, badala yake tukaelekeza nguvu zetu kwenye kupinga udhalimu unaofanywa kupitia uchaguzi shetani. Kushiriki huu uchaguzi shetani, ni kutia muhuri kwenye ushetani mzima unaofanywa na hawa mawakala wa shetani kwenye uchaguzi, ambao hata Nape amekiri kuwa huwa wanafanya ushetani, baada ya huo ushetani eti wanamwambia Mungu awahurumie!! Yaani wanamfanya Mungu kuwa mtani wao!! Hakika kwa haya wayatendao hawataiepa laana ya Mungu. Machoni pa wanadamu wanajiona ni washindi, lakini mbele za Mungu wamelaanika.
Tusipoteze muda wetu kushiriki matendo ya kishetani kwenye hizi chaguzi haramu badala yake tupambane kuuondoa mfumo haramu kwenye chaguzi.