Katika skendo Panama Papers, hakuna wanasiasa ama wafanyabiashara wa Tanzania?

BabaTina

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
429
576
Wadau Habari,

Bila shaka karibu wengi wetu tumesikia kuhusu Panama Papers leak na namna majina ya mastar wakubwa duniani pamoja na political leaders ambavyo wamekuwa wakificha fedha nje ya nchi zao kwa kutumia makampuni fake hali kadhalika kwa kutumia makampuni ya wanasheria wanatumia fursa ya sheria dhaifu katika nchi husika ili kusaidia wahusika kutakatisha fedha ama kuzivusha nje ya nchi.

SWALI:
Katika skendo hii hakuna harufu ya wanasiasa ama wafanyabiashara hapa nchini ambao wameonekana kuhusishwa na scandal hii!?
 
Katika kile ambacho dunia ya kwanza imejiaminisha kuwa rushwa ni nchi za dunia ya tatu tu, sasa Panamagate inawaumbua.

Viongozi wengi duniani hasa kutoka nchi tajiri za magharibi wamegundulika kuiba fedha na kuficha huko nchi ya Panama.
Fedha hizo huingizwa katika kampuni hewa zilizosajiliwa ili tu zifungue akaunti benki kuficha fedha hizo.

Majina ya wahusika ni mengi lakini waliothibitika ni waziri kuu wa Iceland na hata familia ya Cameroon.
Sasa tungependa kusikia toka mashirika kama MCC na utawala bora.
 
Hapa uzuri wenzetu wameibua hii ishu huwa wanafutilia na kuwashtaki na kuwafilisi mali za umma.

Lakini huku kwetu mtu akistakiwa kesi inapotezewa na jinsi kesi inavyoisha hatuelewi mifano tumeona kwenye kesi za Epa na nyingine......
 
Hii mada kwa bavicha ngumu sana kuielewa, maana watu wanajua kile cha bure tu!
kauwezo kako kadogo ka kutafasiri article zilizo andikwa kwa kingereza to kiswahili,hakakupi tiketi ya kujiaminisha kuwa unaelewa kiundani swala la panama papers.
 
Hizo papers ziko zaidi ya milioni kumi na moja. Ni nyingi mno. Kwa hiyo uchambuzi bado unaendelea. Kila nchi inanagalia watu wake walivyohusika. Sijui kama TAKUKURU na Financial Intelligence Unit pale Wizara ya Fedha wanao utashi wa kulifuatilia hili na kutupa taarifa. Linaweza kuipaka serikali yetu tukufu 'matope'. Lakini hata kwenye vyombo vya nchi za Magharibi hili swala linaripotiwa kishabiki. Vidole vimeelekezwa kwa Russia (hasa Putin na washirika wake), China na viongozi wa nchi maskini. Mpaka sasa majeruhi mkubwa ni Waziri Mkuu wa Iceland ambaye amelazimika kujiuzuru. Hapa nchini kashfa zote kubwa zinazohusisha vigogo ziliibuliwa na taasisi za nje kwama Serious Fraud Office (SFO) ya Uningereza na hatua zilizochukuliwa zilikuwa za kutimiza mradi tu. Sijui ni ukosefu wa weledi kwa upande wa wanahabari na wanaharakati wetu? Maana naona hii ni moja ya fursa kwa waandishi/wanaharakati kujizolea sifa kwa kufanya uchunguzi wa kujitegemea.
 
Petro Poroshenko – President, Ukraine
Lionel Messi - Soccer player
Jackie Chan - actor
Salman bin Abdulaziz bin Abdulrahman Al Saud – King of Saudi Arabia
Li Xiaolin – daughter of former Chinese premier Li Peng
Sergey Roldugin – close friend of Vladimir Putin
Arkady and Boris Rotenberg – friends of Vladimir Puti
Ian Cameron – British Prime Minister David Cameron's father
Juan Pedro Damiani – FIFA ethics committee member
Sigmundur David Gunnlaugsson – Prime Minister, Iceland

Hawa ni baadhi yao sijasikia Watanzania
 
kauwezo kako kadogo ka kutafasiri article zilizo andikwa kwa kingereza to kiswahili,hakakupi tiketi ya kujiaminisha kuwa unaelewa kiundani swala la panama papers.
Wewe mwenye kauwezo una hela ngapi Panama?
 
The Power Players · ICIJ
 
sasa messi anahusikaje hapo ni fedha yake halali anayolipwa kwa kiwango chake bora. daah ingekuwa kwa mijiz ambayo inatuibia fedha zetu kupitia siasa
 
sasa messi anahusikaje hapo ni fedha yake halali anayolipwa kwa kiwango chake bora. daah ingekuwa kwa mijiz ambayo inatuibia fedha zetu kupitia siasa
Fikiria kodi anayaikwepa......!
Tufikirie outside the box!
Ni kosa lile lile au baya zaidi alilolifanya mzee wa vijisenti.
 
Hii mada kwa bavicha ngumu sana kuielewa, maana watu wanajua kile cha bure tu!

Hujui lolote mkuu. Na ficha upumbavu wako. Kwasababu hata ulichochangia hata mtoto wa sekondari anaweza kuchangia kizuri zaidi.
 
Fikiria kodi anayaikwepa......!
Tufikirie outside the box!
Ni kosa lile lile au baya zaidi alilolifanya mzee wa vijisenti.

Messi atakwepaje kodi wakati mshahara wake anaolipwa unaingia baada ya kukatwa kodi?

Kinachofanyika kwenye offshore accounts ni wafanyabiashara na makampuni wanakwepa kodi halafu zile hela excess zinaenda kufichwa kwenye hizo nchi zinazotoa tax holidays.

Na pia wanasiasa na viongozi wanaoiba na kufanya biashara, wanatumia mgongo na majina ya rafiki au ndugu kufungua account hewa kwenye hizo nchi.

Kwa muajiriwa kama Messi ni ngumu kukwepa kodi kwasababu mshahara wake unaingia kwenye account yake baada ya kukatwa makato yote.

Labda pesa za matangazo.
 
Does'nt make sense.
Essence ya Panama accounts ni kuficha pato.
Wengine ni halali na wengine si hakali.
Wenye pato lisilo hakali, kuficha inaeleweka, anaficha kipato na anakwepa kodi.
Sasa Messi kuficha pato lake kuna maana gani kama amekatwa kodi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…