Katika siasa, hekima za Freeman Mbowe kama Mwalimu Nyerere

EMACHA

JF-Expert Member
Jul 16, 2021
613
1,169
Ikumbukwe mwaka 1985, Mwalimu Julius Nyerere aling'atuka madarakani huku bado wananchi wengi wakipenda aendelee kuongoza.

Hali hiyo ilijiri wakati nchi ilipokuwa ikikumbwa na changamoto kubwa za kiuchumi kufuatia masharti magumu ya mashirika ya fedha ya Kimataifa (WB na IMF), na miaka michache baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda. Kwa hekima zake, Mwalimu hakusikiliza nyimbo za "mwamba tuvushe," bali alizingatia umuhimu wa mabadiliko ya haraka kwa mustakabali wa taifa.

Hatimaye, alikabidhi uongozi kwa Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Mwalimu pia alijitokeza kwa nguvu kufanya kampeni za kumuuza Mzee Mwinyi kwa wananchi, jambo lililosaidia kumpatia ushindi mnono katika uchaguzi.

Leo, historia hiyo inaelekea kujirudia ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Ni wazi kwamba bado Freeman Mbowe, kama "Mwamba," anakubalika sana ndani na nje ya chama.

Hata hivyo, kwa busara zilezile za Mwalimu Nyerere, kuna kila dalili kwamba Mheshimiwa Mbowe ataridhia mabadiliko ndani ya chama, akimwachia nafasi kinara wa mageuzi, Mheshimiwa Tundu Lissu, ili kukivusha chama katika kipindi hiki chenye changamoto.


Kwa mtazamo wa aina ileile aliyokuwa nayo Mwalimu, Mheshimiwa Mbowe ataibuka na kumkampenia kwa nguvu mgombea Lissu, akimtangaza kama chaguo sahihi kwa wakati huu wa mageuzi.


Hata kama CHADEMA haitachukua dola katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, chama kitasalia imara chini ya nahodha mpya. Vinginevyo, iwapo hakutakuwa na mabadiliko ya uongozi, chama kinaweza kudhoofika.
 
Back
Top Bottom