KWELI Katika picha hii aliyevaa jezi ya timu ya taifa ya Ufaransa ni sanamu ya Kylian Mbappé

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Mdau shiriki kuthibitisha.

Je katika picha hii ni yupi Kylian Mbappe halisi kati ya hawa huku ukibainisha vigezo vya majibu yako.
IMG_20250329_084110_610.jpg
 
Tunachokijua
Kylian Mbappé ni mchezaji wa mpira wa miguu anayependwa na kufuatiliwa na wafuasi wengi wa mchezo wa soka duniani kote anayekipiga katika klabu ya Real Madrid inayoshiriki ligi kuu nchini Uhispania La Liga. Lakini pia ni mchezaji tegemeo wa timu ya taifa ya Ufaransa ambaye alijizoolea umaarufu zaidi katika kombe la Dunia mwaka 2018 ambapo aliweka historia ya kuwa kijana mdogo wa pili aliyefunga goli katika fainali za kombe hilo huku akiendelea kuwa tegemeo pia katika fainali za mwaka 2022 akiwa mfungaji bora wa mabao nane.


Je, katika picha hii, yupi ni Kylian Mbappé Halisi kati ya hawa?

JamiiCheck imekuwa ikiwawezesha wananchi kupata ujuzi utakaowawezesha kufanya uthibitishaji wa maudhui ya picha, video ama sauti ili kuepuka upotoshaji unaoweza kuibuka na kusababisha madhara katika jamii.

Uhalisia wa picha ya Kylian Mbappé aliye halisi kati ya waonekanao katika picha.

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse Image Search ulibaini kuwa picha hiyo ilichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo tarehe 27, Machi 2025 katika tovuti na kurasa za mitandao ya kijamii ya makumbusho ya kihistoria ya Madame Tussauds London, huku Mbappe naye akiichapisha picha hiyo kupitia kurasa zake na kuandika "Let me introduce you my twin"(Nitakutambulisha kwa pacha wangu).

Aidha, Licha ya picha hiyo video iliyochapishwa mtandaoni na Madame tussauds london inamuonesha Mbappe (asiyevaa jezi) akishangaa na kufurahia sanamu yake akibainisha kuwa inafanana kabisa na yeye.

"Ni heshima kubwa, mafanikio makubwa kwangu, na heshima kubwa kuwa sehemu ya familia kubwa ya Madame Tussauds. Asante kwa kila mtu aliyeshiriki katika mradi huu, kwani ni kazi iliyofanywa kwa ukamilifu, na nina furaha sana na matokeo yake."
alisema Mbappe

Hivyo aliyevaa Jezi ya timu ya taifa ya Ufaransa ni sanamu ya Kylian Mbappe kushoto mwa picha hiyo, na hizi ni sehemu ya picha akiikagua sanamu hiyo.
kylian-mbapp%C3%A9-sbs-march-2025_007.jpg
kylian-mbapp%C3%A9-sbs-march-2025_028.jpg
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom