Nyafwili
JF-Expert Member
- Nov 27, 2023
- 4,001
- 9,903
PENZI lilianza kumea kivuli cha utata mkubwa baada ya Baba yangu mdogo kuwa na njaa ya kimapenzi pindi tu alipo fiwa na mke wake wa ndoa, akaona fursa. Ugomvi kati yangu na baba ukawa jukwaa la mapambano ya hisia kali zenye mvutano wa hapa na pale......
House girl ambaye tulizama naye kwenye kisima cha mapenzi mithili ya mwenzi mpevu wa siku 14 ambao umezingirwa na mawingu, hakika nilidhani hakuna mtu yeyote yule atakaye tutenganisha🥰..
Habari wana JF!! Bila shaka ni wazima wa afya baada ya mihangaiko ya hapa na pale, Mwenyezi mungu azidi kuwapa uzima na Afya tele.... Katika maisha kila mwanadamu hupitia majaribu fulani fulani Katika ukuaji wake au Katika uatafutaji 🤝..
Ilikua hivi, Katika ile nyumba ilikua na familia yenye watu takribani saba, kawaida kama tunavyo jua nyumba nyingi za mjini watu wenye kipato nafuu au kilicho juu zaidi hupenda sana kutafuta wasaidizi wa kazi wengine hupendelea wafanyakazi wa kiume au wa wafanyakazi wa kike kutokana na mahitaji yao Katika familia husika. Lakini Katika ile familia ilikua na wafanyakazi wakiume pamoja na mfanyakazi wa kike[House Girl] , kwa sababu baba mdogo alikua na Kazi nyingi ambazo zilihitaji wasaidizi wengi, wengine walifanya Kazi na kuludi makwao lakini wafanyakazi wengine kwa namna moja ama nyingine walilazimika kukaa na boss( baba mdogo) nyumbani kwake,
Kama kijana mdogo niliye zama kwenye ile familia yenye vitimbwi na misuko suko ya hali ya juu iliyo tikisa idara ya ubongo na kata zake kwa pamoja, nikiongezea na kashi kashi mbali mbali za maisha yenye vikwazo visivyo kua na vipimo kule kijijini nilipo zaliwa.
Basi bwana Baada ya kumaliza kidato cha nne shule ya sekondari Kipani, nilitamani sana kuishi mjini kama vijana wenzangu baada ya kumaliza shule huzamia kwenye miji mikubwa kwa ajili ya utafutaji, niliendelea kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki waliopo mjini kuhusu masuala ya kuelekea mjini, hakika nilifulahi sana kusikia vile kwani tangu nizaliwe sikuwahi kufika mjini,
Nakumbuka siku ile ilikua siku ya jumanne nipo na mamaangu mzazi shambani, gafla simu iliita mlio mkubwa kama unavyo jua wazee wanapenda sana kuweka sauti kubwa ili iwe rahisi kwake kusikia, mama alipokea ile simu baada ya kusema halo!!, mama alitabasam na mimi pia ikabidi nitabasam ingawa sikujua anaongea na nani, baada ya mazungumzo yale kuisha, mama alikata simu nakuiweka kwenye pochi ambayo alikua ameivaa shingoni kama kawaida yake.
Haikupita dakika chache ikabidi nimuulize mama ulikua unaongea na nani??? Mama akasimama na kuegemea mpini wa jembe, na kuaza kunihabarisha kuhusu safari ya mjini, kwamba baba mdogo ameniulizia kama nimemaliza shule ili niende mjini, nilitabasamu kusikia ile Habari maana niliona ndoto yangu imetimia, basi tukaendelea na shughuli za pale shambani za kupalilia na kung'oa kunde, mamaangu aliendelea kunisisitiza endapo nitafika mjini nifuate kile kilicho nipeleka na niwe na heshima Katika jamii kwa ujumla, mama akaongezea kusema nasikitika sana kwa kua unatuacha hapa kijijini na wadogo zako peke ake, ambao umri ulikua bado mdogo sana ambao tulikua tumeshibana sana, baada ya kuelezana kuhusu ile safari mama alinitakia kila lakheri kuhusu maisha ya huko mjini, tukaludi nyumbani kwa ajili ya ratiba zingine,
Kufika jioni mida ya saa kumi na moja, kijiji kilikua kimetulia sana huku milio ya Ng'ombe na sauti za Ndege zikitawala, huku baadhi ya wazee nao wakielekea vilabuni ili wakape moja mbili tatu na sisi vijana tuliona ni siku yetu zuri kwa kuwa hakukuwa na mvua hivyo tulijianda kwenda mshambani kwa ajili ya kutafuta kumbikumbi, niliwachukua wadogo zangu nikaungana na kundi kadhaa la vijana pale kijijini, hakika siku ile ilikua zuri sana maana kila mtu aliludi na kumbikumbi,
Haikupita wiki, Wakati ukawadia, ile siku ya kuelekea mjini mchana nikiwa busy kwa ajili ya maandalizi pamoja na kuweka mwili safi maana pale kijijini vijana kuoga ilikua ni mbinde sana , ilipo fika mida ya usiku, mama aliniandalia vifurushi kadha yakiwemo mahindi makavu kwenye kiroba, kunde kwenye kiroba, maharagwe kwenye kiroba na kumbikumbi kiasi kwenye mfuko wa rambo, huku na mimi nikijianda kuweka nguo zangu kwenye begi la shangazi kaja, usiku ule mama alikua na hadithi nyingi sana ambazo zilipelekea kuchelewa kwenda kulala, Nakumbuka siku ile nililala usingizi mzito sana lakini kutokana kile kijiji wafugaji wa kuku, ng'ombe, punda ukiongezea na Ndege pori, hivyo basi ilipo fika mida ya saa kumi na moja, majogoo yaliaza kuwika kwa kupokezana , haikupita dakika kumi nikasikia mlango unagongwa kuku ikifuatiwa na sauiti ikiita NYAFWILI , NYAFWILI... amka ujiandae mda wa safari ume fika, niliamka chapu chapu nakuelekea jikoni ambako mama alikua ananipashia kiporo cha ugali na kunde, mama akaniambia nimekupashia chakula hicho ili njiani njaa isikusumbue, nilinawa mikono na kuaza kula haraka haraka huku mama akitoa mizigo nje ili kuelekea barabarani kusubilia gari linalo toka kijiji cha jirani, tukiwa tuna subiria mda wa Basi kuwasili mama ilikua haipiti dakika tatu lazima aniangalie usoni na kuniuliza HAUONI BARIDI??,
Tulisubilia kama dakika kadhaa hivi tukasikia horn maeneo ya karibu ikiambatana na makelele kama gali lililo choka sana linahitaji matengenezo, basi lilipo fika sehemu tuliyo kuwa tumesimama, mama akasimamisha Basi, Basi likasimama kwa breki ya kusua sua, na konda akafungua mlango huku akiwa ameshika kuluzi iliyo washwa Mwanga mkali, kondakta mwingine akashuka na kigogo kizito alicho kuwa amekumbatia kifuani, baada ya kushuka nacho moja kwa moja akaelekea kwenye tairi la nyuma ya Basi, mizigo ikapakiliwa haraka haraka ili kuwahi wateja vituo vinavyo fuata,, tuliagana na mama angu nikaingia kwenye basi.
Safari ikaanza, huku nikimuombea mama afike salama nyumbani maana mda ule ilikuwa bado giza limetanda, nikiwa mtu Mwenye furaha mchanganyiko na mambo mbali mbali ya pale kijijini na kumuwaza mama angu pamoja na wadogo zangu ambao nilikua nimezoeana nao. Safari ilichukua masaa kadha Mungu ni mwema nilifika salama kule mjini , nikapokelewa kwa bashasha na mama mdogo pamoja na wenyeji ambao sikuwatambua kwa haraka kwa sababu bado nilikua mgeni,
Baada ya mda nikakalibishwa sebuleni ili kimsubili baba mdogo aludi kutoka kazini, mda si mrefu niliskia kelele za gari zikiambatana na honi pamoja na sauti za vijana wakicheka, mfanyakazi mmoja wa kiume baada ya kusikia honi akatoka nje, mara nikasikia shikamo baba, basi yule mfanyakazi wa kiume alifungua geti gari ikaingia na kufunga geti, baba mdogo alipo fika mlangoni akaaza kuniita kwa kiluda NYAFWILI ,,, NYAFWILI,,,, huku akizidi kusogea sebuleni, sura yake ilikua yenye bashasha na furaha ya hali ya juu baada ya kuniona,
Tukasalimiana, bila kuchelewesha mama na house girl wakaanza kubebelea ma-hotpot yaliyo kua yamejaa vyakula na kuyaleta sebuleni, chakula kiliaza kupakuliwa huku tukizungumza mawili matatu kuhusu maisha ya kule kijijini yalivyo , haikuchukua mda baba mdogo na mama mdogo wakaniaga kisha wakaenda kulala, basi ile sebule ikajaa vijana wa Kazi, mtoto wa boss mmoja ambaye alikua darasa la tano na house girl, tukaendelea kupiga story za hapa na pale huku wale vijana wakizidi kunidodosa mawili matatu kuhusu mambo ya kule kijijini nilikotoka, kama unavyojua watoto wa kiume hata kama hamjazoeana story huwa zinaendelea kama kawaida, nilifurahi sana ile siku story zilizidi kunoga huku kiongozi mkuu wa kunogesha story alikuwa ni HOUSE GIRL mwenye macho ya kuita, shape lake kama moto kwenye majani makavu, kila anapo kuangalia kama anakukonyeza vile,,,,
kutokana na ushamba wa TV siku ile sikutamani kabisa kwenda kulala, lakini kwa ya ugeni nililazimika kuafata sheria za ile nyumba, basi yule mtoto wa boss kwa sauti kubwa akasema nazima TV twendeni tukalaleeeee mgeni atakua amechoka sana, dogo akazima TV, baada ya kuzima TV yule mdogo wangu akaniita na kunipeleka chumba cha kulala ambacho kilikua kimeandaliwa kwa ajili yangu.. Tukaagana vizuri huku yule mdogo wangu akisema "usiku mwema kaka, kesho tutaonana mchana maana nitaondoka asubuhi sana kuelekea shuleni" huku nikimuitikia OK sawa masomo mema dogo, mchana tutaonana...
Basi zikabaki sauti za milango kwenye vyumba kadha zikiashiria kila mtu anaenda kulala, isipokua tu kile chumba cha wafanyakazi kiliendelea kuwa na pilika pilika za hapa na pale..
Nikiwa chumbani Niliangaza macho huku na kule, huku nikilinganisha na chumba changu cha kule kijijini kilicho kua cha ajabu kilicho jamaa mashimo mashimo kama barabara ya vumbi iliyo sahaulika na wanasisa kwa muda mrefu.
Nilijilusha kitandani kwa hasira zisizo kuwa na maana, bila kuchelewesha mda nikatafuta shuka la kujifunika na kuelekea kitandani huku nikitoa sauti ya kushusha pumzi "UUHHUMUHHH" , kichwa changu kiliwaza mengi sana hasa kule kijijini kwa mama niliko toka, na huku nikifikiria hatima ya maisha yangu hapo baadae, haikupita mda mrefu usingizi ukanipitia kutokana na safari ile ambayo ilitulazimu kusafiri kwa saa mengi hivyo mwili ulikua umechoka sana.
Kwa mbaali nikasikia sauti na vishindo vikipita koridoni, nikajua tayari kumepambazuka... Baada ya mda mchache kidogo nikasikia pilika pilika za jikoni... Huku bomba za bafuni zikiwa zinatirisha maji kwa pressure kubwa.. Kutokana na uchovu niliokua nao niliendelea kulala kama kawaida, haikupita dakika 30, nikasikia mama mdogo anamuita house girls " SIKITU.. SIKITU" bila kuchelewa naye SIKITU akaitika ABEEE....MAMA huku kwa mbali nikisikia viatu vya mama mdogo vikielekea kule jikoni, nilikua nasikia zile sauti na vishindo vya kwa sababu kile chumba nilicho fikia kilikua karibu na jikoni,
Basi ilikua rahisi kusikia baadhi ya mambo yanayo endelea kule jikoni... nilivyo sikia yule House girl akiitika na kusikia vile viatu vya mama mdogo vikikwaruza chini haikupita dakika chache nikasikia mama mdogo akisema utamsikiliza mgeni wetu, kama kuna chochote anahitaji basi utamuelekezea, SIKITU anaitikia sawa mama....
Nilivyo amka asubuhi nilizima taa ya chumbani kwangu, nikaludi kukaa kwenye kitanda huku nikiwa nimebanwa na mkojo mithiri ya kibofu kuzidiwa, kutokana na hali ya mkojo kunikaba ilinilazimu kufungua mlango na kuelekeza hatua nje,
Lakini kabla sijapiga hatua nyingi nilona kuna mlango mwingine tofauti na wa jana usiku nilio pitia wakati nakuja, nikajisemeza kichwani ngoja nipite huu ili niende nje nikakojoe haraka, lakini baada ya kupiga hatua kadha nikaona kama kuna nyumba nyingine hiyo sehemu ninayo elekea, basi nikageuza fasta sana huku mkojo unazidi kunielemea, nikaaza safari ya kufuata ule mlango wa jana na nikafanikiwa kutoka nje, hakika niliona uzuri wa mji huku wadada wadogo wadogo wenye rika yangu wakipamba ule mji ambao walionekana wamemaliza kidato cha nne hivi na kujiita WANAKIJIJI,
Niliwaangalia kwa macho ya ushamba kama unavyo jua kuku mshamba hawiki mjini, hata akiwika basi sauti haina nguvu, lengo la kukojoa likawa limeshindikana kwa sababu nilitafuta sehemu ya kujificha angalau, lakini watu walizidi kupita na watoto wadogo wadogo walikua wanacheza maeneo yale, ilinilazimu kuludi ndani maana mkojo ulinikaba sana huku matone matone ya mkojo yakindokea kwenye ile suluali ambayo ilivaliwa bila nguo yeyote ya ndani,
Nikiwa nimesimama mlangoni gafla SIKITU nilimuona anatoka jikoni na kuelekea chumbani kwake,, sauti ikasikika shikamo kaka, nikaitikia kwa sauti ya uoga yenye mkwaruzo marahaba... SIKITU akaniambia ukitaka kuoga vyoo na bafu ni vile kule.. Nikamjibu sawa, sikuchelewa baada ya SIKITU kuingia chumbani kwake, nami nikatembea haraka sana kuelekea chooni...
Nilishangaa sana kuona Choo cha namna ile kilichoja marumaru, bomba la maji, kama unavyo jua masuala ya vyoo vya kijijini ni vya kuchimba shimo lefu alafu tunalaza miti kisha maisha yanaendelea wengine walienda mbali zaidi pale kijijini walkua wanaenda kujisaidia polini, basi nilikojoa mkojo mwingi sana ulio nisababishia na kusikia maumivu ndani ya kibofu...nikaludi tena chumbani baada ya kushusha tanki la maji ambalo limenihangaisha kwa dakika kadha,
Baada ya mda kidogo SIKITU akanigongea mlango, nikafungua, nilipo fungua akaniambia mama alisema ukiamka nikupe hii(ilikua taulo), akaongezea kusema maji ya kuoga yapo bafuni, nikaitikia Asante, (hii ndo ilikua safari ya kwanza ya kwanza kuoga asubuhi na jioni), nikaelekea bafuni lakini nilipo fika bafuni ni sikuona ndoo yeyote kama tulivyo zoea kule kijijini kuoga kwa kutumia ndoo au dishi, nikaangaza kwenye dirisha nikaona dodoki/katani na sabuni iliyo nukia sana ambayo ilikua na rangi nyeusi, upande wa kushoto niliona koki zipo ukutani kwa juu kulikuwa na chuma lenye matobo matobo kama chujio hivi, nikafungua koki moja wapo, maji yalitoka mengi sana yakanilowanisha mwili mzima bila kutarajia,,,
Nilivyo maliza kuoga nikaludi tena chumbani ili nisubilie ratiba gani inafuata maana siku ile kulikua kumetulia sana kwa sababu watu walikua wamesha enda kazini kwa hiyo zilibaki sauti za sufuria kule jikoni zikiendelea kupika maakuli, haikupita dakika tatu,SIKITU akaniita kwa ajili ya breakfast, hakukua na maongezi yeyote yale kutokana na ule ushamba nilio kuja nao kutoka kijijini..
Maisha yakaendelea kama kawaida, haikupita wiki mbili baba mdogo akinitafutia kazi kwenye kampuni yake, basi nami nikawa naamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kujiandaa ili kuwahi kazini, kuna mda alikua anatupa lifti kwenye gari yake lakini kuna mda tulikua tunatembea kwa mguu kutokana na sehemu ya ile Kazi haikuwa mbali kiasi hicho, nikazoea maisha ya mjini, nikawa kijana Mwenye kutupia pamba kali, usharo baro ukazidi ukanivaa kila kukicha...
Basi bwana kutokana mihemko ya vijana Kama tunavyojua, nikaaza kutamani watoto wa kike hata mama wa makamo A. K. A mishangazi nilijikuta navutiwa nayo sana, sasa kutokana na swaga zero, DOMO ZEGE🤒 ilikua ngumu sana kumpata mwamke wa aina yeyote ile hivyo nilizidi kuumia na kuendelea kunywa maji mengi kila kukicha 🥴, Binadamu wanasema mungu hamtupi mja wake, kuna siku Katika tembea tembea zangu huku nikiwa nawaza mambo kadha kwa mbali niliona kipande cha gezeti ambacho kilonekana kimenawili mafuta ya maandazi, nikakisogelea nikaokota, maandishi yenye herufi kubwa yaliyo kuwa yamekolewza na wino mwekundu likisomeka (UDHAIFU WANGU NI KWAKO TU 💋) , bila kupepesa macho nilitafuta sehemu nikakaa angalau nipumzike kidogo kutokana na ile sehemu niliyo pita ilikua na kamlima kidogo, nilisoma kile kipande cha gazette kilikua kimebeba ujumbe mzito sana kuhusu mapenzi na namna ya kutongoza 😄, hakika siku ile nilifurahi sana na kujisemea kwa sauti ya usishindi "sasa udomo zege kwisha habari yake" 😐,
Baada ya kusoma kile kipande cha lile gazeti, nilikiweka mfukoni na safari ikaendelea kama kawaida, huku nikiwa napiga piga mateke nyasi na makopo yaliyopo barabarani. Nilivyo fika nyumbani nikapata chakula kama kawaida kilicho pikwa na mtoto wa kienyeji[ ch*uch* saa sita, sauti ya ndege Mwenye rangi mchanganyiko, akitembea mijusi porini inatikisika😄, ] bila kupoteza mda nikaingia chumba cha mdogo wangu nikachuka peni na karatasi tayari kwa ajili kuandika ile mistari iliyopo kwenye gazette ili niaze safari ya kukariri vizuri kabisa bila kuacha hata nukta.
Hii ni daadhi ya Mistari ambayo ilikuwemo kwenye kile kipande cha gazette 😀.
• MACHO YANGU NDO YALIKUONA, MOYO WANGU NDO ULIKUPENDA.
• UDHAIFU WANGU NI KWAKO TU, ILA NIEWAPO NAWE SIJIWEZI KWA LOLOTE LILE.
• MAJI NI MEUPE JAPO HAYANA RANGI, NA PENZI VILE VILE HALINA RANGI.
• NIWAPO NAWE SIJIWEZI KWA LOLOTE LILE, NI SAWA NA MOTO KWENYE MAJANI MAKAVU HAKIKA NI WEWE WA KUNIOKOA.
• NAJUA BAADA YA KAZI ZA MDA MREFU MWILI WAKO UMECHOKA, BASI NAOMBA UFUMBE MACHO UNIWEKE USONI MWAKO, MACHONI PAKO HAKIKA UCHOVU UTAPUNGUA NA KULUDIWA NA NGUVU.
Itaendelea Baada ya siku chache ...... 🙏🙏