Katika marafiki ulio nao wangapi ni marafiki zako?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
7,189
10,366
Kuwa na idadi kubwa ya wanaokushangilia kipindi ukiwa unaelekea kushinda hakumaanishi una marafiki wengi! Siku utakapoupoteza ushindi ndiyo utashangaa kuwa katika watu mia moja ulioamini ni marafiki zako, walio marafiki zako kweli, pengine hawafiki hata kumi!

Inawezekana ofisini kwako unaheshimika sana, lakini siku utakayoacha kazi inawezekana hata aliyekuwa "mdogo" sana kazini kwenu akakuonesha dharau hadharani!

Nilishangaa sana miaka ya nyuma, baada ya kuwa nje ya ajira kwa muda, baadhi ya watu nilioamini ni marafiki zangu hawakutaka hata tena mawasiliano nami.

Nakumbuka mmoja wa marafiki zangu tokea tukiwa sekondari, aliahaidi kuniazima kiasi fulani cha fedha. Lakini nilipomtafuta baadaye kwa ajili ya kumkumbusha hilo, simu yangu haikupokelewa. Nilikuwa nikipiga simu Asubuhi, Mchana, na hata Usiku lakini ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa, na wakati mwingine ilikuwa ikikatwa. Niliamua kutuma sms, lakini nazo hazikujibiwa, japo nilituma zaidi ya mara moja.

Nilipobaini kuwa jamaa kaamua kunikwepa, nilimtumia sms kuwa kuhusu hela niliyotaka kumkopa asisumbuke tena kwani nilishapata suluhisho, lakini hata hiyo nayo haikujibiwa.

Kwa kipindi cha kama miaka miwili hivi hatukuwa tukiwasiliana, japo hapo kabla ya kumshirikisha changamoto yangu, muda ulikuwa haupiti bila ama yeye kunitafuta au mimi kufanya hivyo. Lakini baada ya muda wa miaka miwili au mitatu hivi kupita, alinitumia sms kunisalimia, na mimi nikaijibu kwa amani tu, kwa sababu hata hivyo hatukuwa na uadui. Yeye aliamua kunikwepa kwa ajili ya kuepuka kuniazima fedha zake.

Kipindi hicho hicho, kuna watu ambao nilishawahi kuwasaidia, tena mwingine niliwahi kwenda kukopa hela ili nisaidie kutatua changamoto aliyokuwa nayo. Lakini mimi nilipokuwa nimebanwa, hakuuonesha mwitikio kama niliokuwa nao kipindi alipokuwa na shida. Jibu lake yeye lilikuwa jespesi tu, "nilikuwa nazo ila nimeshaagzia mzigo". Muda huo mimi nilikuwa natafuta hela ya mgonjwa aliyekuwa amelazwa hospitalini, lakini yeye alipokosa hela ya kumalizia malipo chuoni, nilienda kukopa ili tu kumsuport asiahirishe mwaka.

Japo nilikuwa najua kuwa watu huwa wanabadilika kipindi cha changamoto, kipindi hicho ndiyo nilishuhudia kwa ukubwa zaidi!

Marafiki wa kweli hujulikana kipindi cha shida. Pamoja na wengi kunikimbia kipindi hicho, wachache walisimama nami kipindi chote cha "mateso" yangu! Walikuwa hawafiki hata kumi!

Hao ndiyo ninaowaita "marafiki". Hawabadilishwi na mazingira!

Wewe unao marafiki wangapi?
 
Daah mi hapo kwenye marafiki ni kipengele maana kila mtu nacheka nae tuu mi sijui kutunza siri zangu ani mtu wa kufunguka tuu mda wote ndo mana kila mtu najikuta nipo nae deeply...

Naposema mi mtu wa kufunguka sio ndo openly kabisa hapana kuna mambo mengine nipo Very secret

Mfano hakuna mtu anayejua mambo nayotumia in term ya kutega pesa kupitia angel number..

Hakuna mtu anayejua njia nayotumia kutoka na mishangazi hapa gomz.

Lakini kingine ambacho naficha ni wizara nayofanyia kazi
 
Kula stage wanapungua tu..
Kutokana na life style ya kuhama hama sina rafiki wa kusema takaa nae weeeeh hapana
 
There are no Friends but Friends in Need, and whose loyaly is unguaranteed !!! This is the hard fact in the world that we are leaving today !!! So trust nobody !!
 
Kumbe tumo na "Waganda " humu? Tutafsirie basi mkuu?
Ni rafiki zetu ,tunaoshare nao moment zetu nzuri na mbaya tunawaita katika shida na raha Ila mwisho wanatusaliti Hawa ni bayuda Kaka ,sijui utaiwekaje kwa kiswahili ndugu

Bayuda tuyita nabo ,tulala tuseka nabo Ila ni masnitch
 
Kweli sina rafiki zaidi ya mke wangu ambaye na yeye kageuka Kuwa changamoto kubwa sana maishani mwangu!
 
Maisha mazuri ni kutambua kwamba uko hapa Duniani peke yako, kuwa a good person si kitu kibaya lakini ni kujitolea tu lakini sio lazima.
 
Kweli? Wanaweza wasiwe wengi lakini siyo rahisi umkose hata mmoja.
Kuna washkaji tu. Sio rahisi kuwa na rafiki kwa dunia ya sasa.

Kila mtu atakuwepo kwa sababu ya kitu fulani ila sio kwa ajili ya kuwa na bond isiyovunjika kama ile iliyotajwa na Wiz Khalifa kwenye see you again.
 
Back
Top Bottom