Kazi ya upinzani sio kupinga, kukosoa na kuonyesha udhaifu wa serikali tu, hii ni kazi nzuri sana. Lakini kikubwa ni kuonyesha taifa mbadala wa hiki tunachokiona.
Ajitokeze UKAWA mmoja shupavu atoe speech inayoonyesha mbadala wa jumla wa hiki tunachokiona. Ninachokiona kikubwa ni kujenga hoja huku msingi wa hoja ni makosa au maamuzi ya Mtawala aliyepo.
Nje ya hapo Sioni Solid base ya UKAWA na mbadala wa jumla kwa hiki tunachokiona. Wakati nchi iko katika maswali mengi na upenzi wa kishabiki hii ninaiona kama fursa kubwa kwa wapinzani kutuonyesha kwanini wao na sio CCM ila wamelala, wengine wanalialia na kurukiarukia vimatukio.
Hapa mnakera kiasi hasa wapenzi wa mabadiliko ya kweli.