Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,395
- 6,617
Serikali imeeleza kuwa moja ya changamoto kubwa inayoikumba mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania, ikiwemo Arusha, Manyara, Kilimanjaro, na baadhi ya maeneo ya Tanga, ni upungufu wa msongo wa umeme (voltage drop), hali inayosababisha mwanga hafifu wa taa na kushusha ufanisi wa vifaa vya umeme majumbani na viwandani.
Akizungumza mkoani Dar es Salaam siku ya Jumatatu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba, amesema kuwa tatizo hilo linatokana na umbali mrefu wa kusafirishwa kwa umeme kutoka vyanzo vikuu vya uzalishaji vilivyopo Kusini mwa mikoa hiyo ya Kaskazini.
"Umeme mwingi wa Tanzania unazalishwa Kusini, katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, na Iringa. Ili kufika Kaskazini, umeme huu unasafiri hadi kilomita 700 kwa baadhi ya maeneo, na safari hii ndefu husababisha kupungua kwa nguvu za msongo wa umeme (voltage drop) kabla ya kufika kwa mtumiaji wa mwisho," ameeleza Mramba.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, upungufu wa volteji husababisha upotevu mkubwa wa umeme njiani, jambo ambalo linachangia kuongezeka kwa gharama za usambazaji wa nishati hiyo na kudhoofisha maendeleo ya viwanda katika mikoa hiyo.
Ili kutatua tatizo hilo, Serikali imepanga kuingiza umeme mpya kutoka Ethiopia kupitia mpaka wa Namanga. Makubaliano kati ya Tanzania na Ethiopia yameshafanyika, na utekelezaji wa mpango huu unatarajiwa kuleta maboresho makubwa katika sekta ya nishati, hasa kwa wananchi wa Kaskazini.
"Tunataka kuhakikisha kuwa msongo wa umeme unaimarika katika mikoa ya Kaskazini kwa kuongeza chanzo kingine cha umeme. Umeme huu kutoka Ethiopia utasaidia kuinua volteji iliyo dhaifu, kupunguza upotevu wa umeme, na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zaidi," amesema Mramba.
Soma, Pia