Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Nchimbi aweka shada la mauwa kwenye kaburi la Shujaa Magufuli, ammwagia Sifa za Utumishi Uliotukuka!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
90,246
156,575
Ni jambo jema

Kanisa Moja Takatifu La Mitume

Mlale Unono 🌹🌹
---

1723497801288.png
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa kazi kubwa anayoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiyo namna sahihi ya kumuenzi Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli.

Balozi Nchimbi amezitaja mojawapo ya kazi hizo kubwa zilizofanywa na na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ni kuendeleza na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya kitaifa kwa ujumla na mingine katika Mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato, iliyoanzishwa wakati wa uongozi wa Rais Magufuli.

Katibu Mkuu wa CCM amesema hayo leo Jumapili Agosti 11, 2024, wakati wa sala fupi ya kumuombea Hayati Magufuli iliyofanyika kwenye kaburi la kiongozi huyo.

Vilevile, Balozi Nchimbi alirejea maneno yake hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Stendi ya Zamani, mjini Chato, akitaja baadhi ya miradi, ikiwemo ujenzi wa Treni ya Kisasa (SGR), Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere na jinsi ambavyo Serikali inayoongozwa na Rais Samia imeshusha kiasi cha Sh. 123 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Chato.

Hapo awali, wakati wa mapokezi ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ulipokuwa ukiingia Mkoa wa Geita, ukitokea mkoani Kagera, katika Kata ya Muganza, aliwasisitiza wananchi wa eneo hilo umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kama alivyokuwa Rais Magufuli, ikiwa ni mojawapo ya njia nzuri za kumuenzi.

Balozi Nchimbi amesema yeye na msafara wa viongozi, wakiwemo Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM aliombatana nao, wamefarijika kufika mahali hapo alipozikwa kiongozi huyo, ikiwa ni mojawapo ya njia ya kumuenzi kwa uongozi wake alioutoa kwa CCM na nchi kwa ujumla.

“Sote ni mashahidi na tunatambua mchango mkubwa wa Hayati Magufuli kwa Chama chetu na nchi yetu. Kazi hiyo kubwa aliyofanya iliashiria uzalendo mkubwa aliokuwa nao. Nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, hasa kwa kuendeleza miradi yote iliyoachwa na hayati Magufuli, ikiwemo ya Mkoa wa Geita na Chato, kama alivyosema Mbunge,; amesema Nchimbi
 
Weka hata trillions of mashada, katili limekufa , limeoza kwisha habari yake! I
Ukatili kwa watu haulipi, utaandika historia ambayo haitafutika. na CCM ikiondoka madarakani, upuuzi huo utabaki kwa ndugu zake! SAMIA weka historia yako vema sasa! Wapambe wanakudanganya! Akili za kuambiwa changanya na zako
 
Retired straight man now officially gay
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa kazi kubwa anayoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiyo namna sahihi ya kumuenzi Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli.
Ingawa alichosema hapa ni kweli, lakini wanasiasa ni watu wanafiki sana 😢
 
Back
Top Bottom