Wasalaam Kilimo-Tz
Kama ilivyo slogan ya serikali ya Tz katika kuendeleza uti wa mgongo wa taifa "KILIMO KWANZA" na mimi kama walivyo wadau wengine napenda kuwatambua watu mbali mbali ambao wanaitendea haki slogan hii ya taifa"KILIMO KWANZA"
Dr. Kisa Mtaalam wa Kilimo kutoka Idara ya Maendeleo ya Mazao ni jembe. Dr Kisa ameonyesha ukomavu katika utumishi wa umma kwa kujituma katika kuhakikisha kwamba miradi mbalimbali ya kuendeleza kilimo inafikia lengo lililokusudiwa. Ijapokuwa Dr. Kisa ni mwanamke kama walivyo wanawake wengine katika uongozi Dr. Kisa amekuwa ni mtu wa kufocus kwenye kazi yake, si mtu wa kusikiliza majungu na amekuwa mtumishi ambaye anakaa mbali na skendo yoyote ya kuvunja kanuni na maadili ya utumishi wa uma.
Dr. Mansoor yeye sina hata haja ya kumuelezea, ukikutana naye tu kwa bashasha na ukarimu aliokuwa nao utagundua ni mtu anayejua nafasi aliyopo. Dr. Mansoor ni mtu anayejua kujenga hoja, amekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya watumishi waliopo chini yake, uadilifu, uaminifu na kusikiliza maoni ya watumishi wenzake zimekuwa ni nguzo muhimu kwake katika kufanikisha ustawi wa maendeleo ya utafiti wa mazao ya kilimo.
Katibu Mkuu tafadhali watumie sana hawa wataalam wako.