Katibu mkuu CWT agoma kurudi Temeke kufundisha

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
577
2,594
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imeanza mchakato wa kufungua shauri la nidhamu dhidi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japhet Maganga baada ya kutorejea katika kituo chake cha kazi tangu alipotakiwa kufanya hivyo Oktoba Mosi mwaka huu.

Maganga ambaye cheo chake ni Mwalimu Mwandamizi katika Manispaa ya Temeke, aliomba kibali cha kuazimwa kuitumikia CWT Agosti 2017 hadi Septemba 30, 2020, akaomba tena Juni 1, 2020 na kumalizika Septemba 30, 2023, na baadaye aliomba kibali hicho kwa mara ya tatu lakini Katibu Mkuu UTUMISHI hakuridhia maombi hayo na kumtaka kurejea kwenye kituo chake cha kazi cha awali.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya amesema Maganga ni mtumishi wa Temeke na alitakiwa kuripoti kazini kama alivyotakiwa katika tangazo la wito, lakini hadi sasa hajaripoti, hivyo kinachofanyika ni kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake.

"Yule ni mtumishi wa Serikali hapaswi kuigomea Serikali, sisi tunachojua yeye ni mtumishi wetu, kule aliko kibali kimeisha sio tena sehemu yake ya kazi, amesema.

Maganga alichaguliwa Desemba 2022 na Mkutano Mkuu wa CWT kuwa Katibu Mkuu akichukua nafasi ya Deus Seif
ambapo awali alikwa akitumikia nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.

Mnamo Januari 25, mwaka huu, Maganga, Makamu wa Rais wa CWT, Dinna Mathaman na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Wakuu wa Wilaya lakini Maganga na Mathaman hawakufika kuapa.

Swahili Times.

Pia soma:
 
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imeanza mchakato wa kufungua shauri la nidhamu dhidi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japhet Maganga baada ya kutorejea katika kituo chake cha kazi tangu alipotakiwa kufanya hivyo Oktoba Mosi mwaka huu.

Wameamua kumkomalia kisa kukataa teuzi, sio kila mtu ni mtumwa wa teuzi, waache ushamba.
 
Wameamua kumkomalia kisa kukataa teuzi,sio kila mtu ni mtumwa wa teuzi,waache ushamba.
Ndiyo hiyo. Ila ni vizuri ili watu wazidi kujifunza na kuacha kuwa vibaraka wa serikali. Hivi vyama vya wafanyakazi badala ya kutetea wafanyakazi viongozi wake wamegeuka vibaraka wa serikali. Hakika kila mtu ataonja balaa la utawala huu mbovu, unaokomoa kila mtu anayekwenda kinyume nao mpaka tujikubali kuwa tatizo ni CCM na tuungane kuiondoa.
 
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imeanza mchakato wa kufungua shauri la nidhamu dhidi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japhet Maganga baada ya kutorejea katika kituo chake cha kazi tangu alipotakiwa kufanya hivyo Oktoba Mosi mwaka huu.

u CWT aliyekataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya arudishwa kwenye Ualimu
Nafikiri sheria za utumishi wa umma, usiporejea kazini ndani ya saa 72 bila ruhusa unakuwa umejifukuzisha kazi. Hapo hakuna haja ya kupoteza hela ya walipa kodi kuanza kumzungumzia mtumishi wakati Sheria zipo straight. Afukuzwe kazi serikalini basi
 
Back
Top Bottom