Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,828
- 13,585
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha ADC, Doyo Hassani Doyo anatarajia kuchukua fomu ya kugombea Uenyekiti Taifa, Juni 11, 2024.
Doyo anakwenda kumrithi Mwenyekiti Taifa, Hamad Rashid aliyemaliza muda wake Kikatiba.
Amesema lengo kuu la kugombea nafasi hiyo kuwa ni kuleta mabadiliko ya Sheria, hali ya ajira na maisha bora kwa kila Mtanzania lakini pia nimekomaa kisiasa.
Amesema "Kipekee nimshukuru Mwenyekiti wa Chama Taifa, Hamad Rashid Mohamed kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa sababu amenifundisha Siasa kwa kipindi cha miaka 10."
Amesema viongozi wengi wanapenda kung'ang'ania madaraka lakini kwa Mwenyekiti wetu ni tofauti ni Mwanasiasa aliyeonesha mfano wa kuigwa kwa Watanzania.
"Ifike hatua nafasi unayopewa na wenzako lazima ufate Katiba ya nchi nina imani Wanasiasa wengine watafuata nyayo za Hamadi Rashid ili kuacha wanachama wapya ili kuweza kufanya kazi," amesema Doyo.
Aidha, amemkaribisha Msingwa kuhamia Chama cha ADC kwa lengo la kuongeza nguvu ili kiwe chama cha ushindani.
Amesema "Juni 20 nina safari ya kuzunguka ili kutafuta Wadhamini watakaonidhamini ili niweze kushinda, ni lazima ni pate wadhamini wasiopunguwa 150, kutoka Zanzibar ni 75 na 75 kutoka Tanzania Bara, katika hao Wadhamini 65 lazima wawe Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa.
"Nimefurahi kwamba uongozi wa chama umenipa baraka katika nafasi yangu niliyotangaza. Sababu kubwa ni kwamba tayari nimejifunza vitu vingi kutoka kwa Hamadi Rashid nimefanya nae kazi kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo.
"Nawahakikishia Watanzania na kuwatoa hofu Wananchi na Watanzania wote ahadi yangu ni kwamba tunakwenda kukiimarisha chama kwa ngazi ya juu."