LGE2024 Katibu Mkuu ACT Wazalendo, Ado Shaibu: Maendeleo haya Chama, wekezeni katika kiongozi bora

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,103
2,633
Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu , amewataka wananchi wa Kijiji cha Katanda, Kata ya ML. Magharibi, Jimbo la Tunduru Kaskazini, mkoani Ruvuma, kuzingatia vigezo vya uongozi bora badala ya kushikilia itikadi za vyama vya siasa wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Ado ametoa wito huo Novemba 25, 2024, wakati wa mkutano wa kampeni za chama hicho kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

"Maendeleo hayana chama. Tukitaka kuendelea, wote wimbo wetu uwe 'Tunduru kwanza, vyama baadaye'. Hata hapa Katanda, wimbo wenu uwe huohuo: Katanda kwanza, vyama baadaye. ACT wakileta mgombea mzuri mchagueni, CCM wakileta mgombea fyongo wapigeni chini. Hata sisi ACT tukiharibu mbele ya safari, tupigeni chini. Kwenye maendeleo hakuna chama, unaangalia siasa safi na kiongozi bora, ndipo unapata maendeleo." Amesema Ado.

Katika mkutano huo, mgombea uenyekiti wa kijiji cha Katanda kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Hassan Shabo, amewaeleza wananchi dhamira yake ya kushughulikia changamoto zinazowakabili kijijini hapo. Ameahidi kuboresha huduma za zahanati, sekta ya elimu, na fursa za michezo kwa vijana.

"Nimeomba nafasi kugombea uenyekiti wa Kijiji cha Katanda ili nitatue changamoto ambazo zimekuwa kero, hususan kwenye zahanati, elimu, na michezo kwa vijana. Nikishindwa kutekeleza ahadi zangu, Katibu Mkuu Ado, njooni mniondoe mwenyewe." Amesema.

Ameendelea kwa kusema kuwa moja ya vipaumbele vyake ni kujenga uwanja wa kijiji kwa ajili ya michezo na kuhakikisha huduma bora zinapatikana katika zahanati ya kijiji hicho.

 
Back
Top Bottom