Oscar Wissa
Senior Member
- Sep 5, 2018
- 107
- 170
Maswali yamekuwa mengi kuhusu jambo hili, Je, Kanisa liitii serikari au serikari itii kanisa? Je, Kanisa linaweza kuwa upande wa chama fulani? Je, serikali inatakiwa kuwaongoza waumini hata katika masuala ya imani?
Mimi nimeona vema kuandika kidogo kuhusu mada hii, baada ya kusoma maneno ya Yesu Kristo mwanzilishi wa kanisa, anaposema, "vya Kaisari mpeni Kaisari, na vya Mungu mpeni Mungu". Aliwajibu jambo hilo maadui zake waliokwenda kumjaribu kwa kumuuliza swali kama ni halali kulipa kodi kwa Kaisari. Kaisari alikuwa anawakilisha Serikari na Mungu anawakilisha kanisa.
Uhusiano kati ya kanisa na serikari ulianza kuelezwa tangu Agano la Kale. Wafalme na waamuzi walikuwa na kazi ya kuongoza katika masuala ya kiserikali. Lakini makuhani na manabii walikuwa wanawaongoza watu katika masuala ya kiimani, kila wakati, mwingine alipoingilia majukumu yasiyo yake, kuna onyo kali kutoka kwa Mungu lilitokea.
Maswali yapo mengi kwenye vichwa vya watu, inakuaje mhubiri anakuwa mwanasiasa? Inakuwaje mwanasiasa anakaribishwa madhabahuni kama mhubiri? Inakuaje kanisa linatumiwa na chama kunadi mgombea?
Sina majibu ya moja kwa moja leo, ila nataka nikupe mwanga kidogo kuhusiana na mambo hayo ninapofafanua uhusiano uliopo kati ya kanisa na serikari.
↪️ Kanisa linahusiana na serikari kwa njia hizi;
1️⃣ Kanisa linatakiwa kuiombea serikari. 1 Timotheo 2:2
Waumini wanatakiwa kuomba Mungu awape viongozi kutawala kwa haki, amani na utulivu. Kuomba ulinzi wa Mungu katika mipaka na kila eneo katika nchi.
Maombi hayatakiwi kuwa ya kisiasa au yaliyojikita katika kupendelea chama fulani, kanisa halina chama. Kuna mtumishi mmoja aliambiwa na Mungu amwombee Iddi Amini, yule mtumishi alipata utata sana katika kuuelewa moyo wa Mungu wa upendo hata kwa wenye mamlaka wanaofanya maovu kwa wanachi wao.
2️⃣ Kanisa linatakiwa kuitii serikari kwa mambo yote, yasiyokinzana na imani ya wokovu. 1 Petro 2:3, Warumi 13:1
Kila aliyeokoka anatakiwa kulipa kodi, kulipa hela za takataka, sungusungu, na kadhalika. Kanisa siyo chombo cha kupindua serikari, bali ni chombo cha kupindua ufalme wa giza. Serikari ilipodai kodi wakati ule wa Yesu na Mitume, Yesu akamwambia Petro akavue samaki, halafu ndani ya samaki kuna sarafu ambayo akiichukua akalipe kodi.
3️⃣ Kanisa halitakiwi kuitumia madhabahu kama jukwaa la kunadi chama au kunadi mwanasiasa fulani.
Manabii wa uongo wakati ule wa Ahabu walikuwa wanasiasa sana hahaha, walimdanganya mfalme ili tu waweze kupata nafasi kwenye moyo wake, wanasiasa mara nyingi wanapenda kusikia mambo wanayopenda kusikia kutoka kwa wafuasi wao wa karibu, "chawa wao". Sasa kanisa halitakiwi kuwa chawa wa serikari, bali linatakiwa kuwa "mwombezi, mshauri na mkosoaji". Nazungumzia kukosoa serikari, sio kukosoa chama.
Madhabahuni ni mahali pa kumhubiri Yesu Kristo na kazi yake iliyomalizika msalabani tu, na si vinginevyo. Ole wenu mnaotumia madhabahu kuwatangaza wanasiasa na vyama vyao, hukumu yenu imeiva!
4️⃣ Kanisa linatakiwa kuishauri serikari
Mara nyingi serikari imekuwa ikiwaita viongozi wa dini na watumishi wa injili kutaka ushauri. Sasa, si kila anayeitwa kwenda kushauri kwamba ushauri wake unatoka kwa Mungu, wengine ni watu wa dini tu ila sio wa injili. Watu wa Injili hasa ambao Mungu ndio anawatambua kama kanisa ndio ambao nawazungumzia. Wanatakiwa kuishauri na kuikemea serikari kwa lugha ya kibiblia. Kanisa lina wajibu wa kuiambia serikari, mapenzi ya Mungu kwa nchi ni nini?. Serikari ina wajibu wa kusikiliza na kutii ushauri wa watumishi wa Mungu, ushauri ule unaolenga kuleta amani, haki, umoja, utulivu na mshikamano. Wafalme na viongozi wengi waliokataa ushauri wa watumishi walikuwa na mwisho mbaya, akiwemo Belshaza, ninawaombea mema viongozi wa Tanzania yasiwakute hayo.
Kanisa kuishauri serikari inaweza kuleta matatizo wakati mwingine, mfano, Yohana Mbatizaji alipoikemea dhambi ya mfalme Herode, mfalme akamfunga Yohana hatimaye akamkata kichwa. Lakini Yesu alimsifia sana Yohana akasema ni nabii mkuu, naam, hakika "tunahitaji manabii wa namna hii wasiojipendekeza kwa serikari", tumepungukiwa sana wahubiri wa aina hii wasio chawa wa serikari.
⏭️ Uhusiano wa kanisa na serikari ni uhusiano unaohitaji kila mmoja akae kwenye wajibu wake na nafasi yake. Kanisa ni mtumishi wa Mungu na serikari ni mtumishi wa Mungu ikiwa tu kila kimoja hapo kitatimiza majukumu yake kwa nafasi yake kama ilivyoagizwa na Mungu.