Kati ya ndoa na ujenzi nianze na kipi?

ContinousImprovement

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
290
268
Wanabodi habari za Muda huu.

Naomba kwa wale wenye uzoefu na walionitangulia katika haya mambo naomba tufahamishane ni kipi muhimu kuanza nacho kati ya Ndoa au Ujenzi wa Nyumba?

Tushauriane tafadhali...
 
Nakumbuka mzee wangu aliniambia unataka kuoa then uje umlaze wapi unataka mimi na mke wako tupishane na mataulo kwenye corridor naenda bafuni? jiulize kwa nini watu wa kaskazini wanaenda kujenga kwanza home then hapa mjini.
 
Apataye mke (Mke sahihi) apata kitu chema, nae ajipatia kibali mbele ya Bwana.

Kuna watu wanamaghorofa wanatamani wayakimbie kwa kukosea kuoa mtu sahihi.
Kama umejiridhisha OA nyumba utajenga nyingi tu kama uko na mtu sahihi. Kama bado unamashaka endelea na ujenzi
 
Wanabodi habari za Muda huu.

Naomba kwa wale wenye uzoefu na walionitangulia ktk haya mambo naomba tufahamishane ni kipi muhimu kuanza nacho kati ya Ndoa au Ujenzi wa Nyumba?

Tushauriane tafadhali...
Mkuu, Nenda sambamba... usianze na jengo!! gawa na ubalance bajeti yako!!
Mke uwenae na jengo uanze poelpole (kiwanja na msingi) huku maisha yakisonga mbele.....
kila la kheri
 
Kuoa kwanza ndio upate mwongozo sahihi,nyumba kujenga ni rahisi ila kupata mke mwema ni bahati
Nani kakwambia? Kipi kati ya Ndoa(Mke) na Nyumba unaweza kutoa talaka na kuachana nacho?. Anza na kile ambacho huwezi kukitolea taraka kwanza. NYUMBA NDO KILA KITU.
 
nakumbuka mzee wangu aliniambia unataka kuoa then uje umlaze wapi unataka mimi na mke wako tupishane na mataulo kwenye corridor naenda bafuni? jiulize kwa nini watu wa kaskazini wanaenda kujenga kwanza home then hapa mjini
Kuna nyumba zkupanga co kwamba ukioa hujjenga utampeleka mkeo kwenu
 
Uombe na Usali kwa Mungu kukupa Mke Mwema. Ukioa either mke amekukuta na nyumba au mlijenga wote, mkiachana itabidi mgawane mali, inaweza kupelekea nyumba kuuzwa na hawa mabinti wanajua kweli kuhesabu baada ya ile miaka miwili ya kuishi pamoja kisheria mahakamani ndio hesabu inaanza hapo.
 
Vyote muhimu unategemea aina ya mchumba
1. Kama ni mchumba bi shoo anza na ujenzi kwani hawezi kuwa msaada hata ktk ujenzi wenyewe
2. Kama mchumba ni mchakarikaji anza na ndoa kwani atakusaidia hata kusimamia ujenzi wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…