Salaam, shalom!!
Kuelekea uchaguzi mkuu 2025, tayari tumekwisha ona homa ya Uchaguzi, HOFU kubwa ni kutoboa na kupata ushindi 2025. Wapo watia Nia ambao wamekwisha Anza compaign kabla ya Uchaguzi katika nafasi mbalimbali, yote hiyo ni homa ya Uchaguzi.
Homa hiyo hiyo Iko katika ngazi zote, Udiwani, ubunge na Urais.
Wananchi ni Kweli wameichoka CCM, pia wamechoshwa na undumilakuwili wa baadhi ya vyama kinzani, lakini Kuna wakati wananchi wamekuwa wakipiga kura Kwa chama Fulani Kwa kuangalia mgombea.
Yaani Kuna wakati wagombea wanavibeba vyama Kwa kukubalika kwao Kwa wananchi bila kujali chama kilichompa ridhaa kugombea.
Unakuta Mwananchi katika karatasi ya kura, anamchagua Kwa Mfano, Diwani Kutoka CCM, Mbunge Kutoka CHADEMA, na Rais Kutoka chama kingine, CHAUMMA. Uchaguzi wa aina hii, huangalia ubora wa mgombea bila kujali chama chake anachokiwakilisha.
Kwa yaliyotokea 2020 na yanayoendelea sasa, vyama vinakwenda kukumbana na Hali hiyo, Hali ya wananchi kuviadhibu vyama ikiwa wataletewa mgombea wasiyemtaka.
Kwa kulijua Hilo, CHADEMA mara zote katika nafasi ya Urais, imejizuia kutangaza mgombea wao na kusubiri kwanza waone mgombea wa washindani wao chama Cha MAPINDUZI. HOFU ni hiyo hiyo kutafuta mgombea anayekubalika zaidi na wananchi.
Kuna wanaosema kuwa Eti ukipitishwa tu CCM, basi umejihakikishia ushindi, hili Si Kweli hata kidogo, yaliyotokea 2015 ni darasani tosha.
Nauliza tu Kwa Mfano, ikitokea kuwa Mtarajiwa au anayepewa nafasi kugombea Kwa tiketi ya chama Cha MAPINDUZI au upinzani Kwa Mfano, amekosa mvuto mbele ya JAMII, je chama kitashupaza shingo na kukubali kupoteza ushindi, au kitaamua KUBADILI mgombea Ili kupata uungwaji mkono wa wananchi?
Karibuni🙏