Kati ya Biashara nyingine, Voda-wekeza, UTT na Mabenki kwa wale wazoefu ni kipi unaweza mshauri mtu awekeze ?

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Jan 9, 2022
1,212
2,622
Habari JF , kuna kipindi nliwahi anzisha uzi ambao lengo lake lilikuwa ni kujua ni nani hasa mmiliki wa UTT , nlipata majibu mengi ambayo yalinirodhisha kwa Asilimia kama 70 .

Najua biashara ina risk zake , Voda, UTT kwa kiasi chache Tunawajua wamiliki .

Mabenki iko wazi umiliki wake .

Kwa mlio wahi wekeza pesa sehemu mnashauri nini ? Au bora biashara nyingine?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

Prof. Faustin Rweshabura Kamuzora ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Uwekezaji ya UTT – AMIS. Prof. Kamuzora ni Katibu Tawala wa Mkoa Mstaafu, anachukua nafasi ya Bw. Casmir Kyuki ambaye amemaliza muda wake;

Prof. Joseph Andrew Kuzilwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP). Prof. Kuzilwa ni Profesa Mstaafu, Chuo Kikuu cha Mzumbe; na

Prof. Ahmed Mohamed Ame ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kwa kipindi cha pili.

Uteuzi huu umeanza tarehe 04 Agosti, 2024.

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom