JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,696
- 6,491
Meleji Mollel ambaye ni Afisa Hifadhi Katavi na Daniel Walakunga ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo wamesema shughuli za uvuvi zinazingatia maelekezo ya mipaka ambapo vibali vyote haviruhusu kuingia katika hifadhi ya Katavi.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf amesikitishwa na wananchi hao kutofanya shughuli hiyo ipasavyo ambapo ameagiza pesa walizotoa kwa ajili ya kupewa vibali zirudishwe kwa wananchi haraka.