Katavi: Mganga Mkuu wa Wilaya asema wapo kwenye mchakato wa kuajiri Mhasibu wa Hospitali ya Wilaya ya Mlele

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,938
13,696
thumb_781_800x420_0_0_auto.png
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi, Dkt. Thadeus Makwanda ametoa ufafanuzi kuhusu hoja ya Mwanachama wa JamiiForums.com aliyeeleza kuwa Hospitali ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi haina Mhasibu hali ambayo inaweza kusababisha upotevu wa fedha na kuwa Watumishi wasio na taaluma hiyo ndio wanatumika kupokea fedha zinazoingizwa Hospitali.

Kusoma zaidi alichoandika Mwanachama huyo, bonyeza hapa ~ Hospitali ya Wilaya ya Mlele – Katavi haina Mhasibu, watumishi wa kawaida ndio wanapokea fedha za Wagonjwa

UFAFANUZI WA MGANGA MKUU WA WILAYA
Akifafanua hoja hiyo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi, Dkt. Thadeus Makwanda anasema:

“Tayari tupo kwenye mchakato wa kuajiri, huwezi kumuajiri mtu bila kuwa na bajeti, hospitali ni changa haikuwa na mapato, Wahasibu wanaajiriwa na Serikali Kuu na kwa kuwa ajira hazitoki sana, Hamashauri tumeshalifikiria hilo na tumeshatenga bajeti.

“Watumishi wa kawaida wanapofanya shughuli hizo za Uhasibu kuna muda wanakwama kufanya majukumu yao mengine ndio maana tumetenga bajeti ili tuajiri hata Mhasibu kwa Mkataba na Mkurugenzi amesharuhusu mchakato huo uendelee.

“Utaratibu wa sasa hakuna fedha ambayo mtumishi anakaa nayo, kila kiasi kinachoingizwa kwa maana ya kufanyika malipo kiasi kinapelekwa benki, hakuna mtu anayekaa na fedha mkononi.

“Unajua tuna Wakaguzi wa Nje, wanakuja kila mwaka hawawezi kukubali fedha zikae mkononi.

“Pia, kuanzia mwezi huu wa pili, vituo vyote tumefunga mfumo ambao utamwezesha mlipaji kutumia Namba ya Malipo.”
60756ad4ed405082086545.png
 
Hivi Halmashauri ya Mulele ata Bilioni moja ya Maputo ya ndani wanaweza kuikusanya?
 
Back
Top Bottom