Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,735
- 13,498
Rehema akiwa katika hospitali hiyo akipatiwa huduma ya matibabu alikwenda chooni kwa lengo la kujisaidia ndipo uchungu ukamkuta huko na kujifungua mtoto wa kiume akiwa mzima, ndipo akafanya jaribio la kumuua kwa kumuingiza kwenye tundu la choo na hatimaye akamuweka kwenye sinki la la maji na kumtelekeza hapo na kurudi wodini.
Imeelezwa kuwa Rehema aliondoka Katavi Augusti 2023 kuelekea Dar, akarejea Novemba 2023 ambapo Desemba 2023 alipata mchumba na kuolewa, hivyo alitoa mimba ili kuokoa ndoa yake na mumewe asijue kuwa alimuoa akiwa mjamzito.
Bibi wa kichanga hicho ambaye ni mzazi wa Rehema amesikitishwa na tukio hilo la mwanae kufanya uamuzi wa namna hiyo.
Dr Gloria Solo ambaye ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo amesema mtoto amekutwa amevunjwa miguu na majeraha mbalimbali katika mwili wake ambapo amesema hali ya mtoto inaendelea viziri huku Afisa Ustawi wa Jamii Telesis Mwendapole akieleza namna mtuhumiwa huyo alivyojaribu kuua kichanga chake.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusufu amesema kitendo kimechofanywa na Rehema hakikubaliki ndani ya jamii ambapo ameagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria dhidi yake huku akisisitiza Wazazi na walezi kutowatuhusu Watoto wa kike kuolewa wakiwa na umri mdogo.