Lakasa chika7
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 454
- 1,264
Tuelekeze ilipo irrigation system yako tuje tujifunze.Mungu alimuumba MTU akampa akili, ufahamu, ujuzi, taalamu na maarifa. Ndo maama leo mtu akiumwa hatakiwi kwenda kanisani na msikitini kuombewa anatakiwa aende hospital akatibiwe. Mungu aliumba utaalamu na ujuzi wawa kutibu na kutambua magonjwa na kuyaponya kwa binadamu ambao tunawaita madaktari. ukiona unaumwa nenda hospital ukapate tiba. Ukiombewe bila kwenda hospital utakuwa unakufuru na utakufa tu kwakuwa mungu alimuumba binadamu kwa kufanana naye. Mungu kampa mwanadamu akili na maarifa ya kufanya vitu vingi indirectly ili ujuzi huo usaidie wanadamu.
Leo mwanasiasa anatuambia tuombe..au mwanasiasa anahimiza viongozi wa dini wafunge/ waombe.
Eti tuombe kwa Mungu maombi mazito Mungu alete mvua. Kufanya hivyo ni kumkosea sana Mwenyezi Mungu. Mungu ametupa akili ya kutambua mabadiliko yq hali ya hewa na adaptation measure za ku overcome hizo demerits za climate change.
Mabadiliko yq hali ya hewa yanasababisha kutokuwepo kwa mvua. Na suala la mvua kupungua litaongezeka sana tena sana tu.
Zipo njia nyingi ( adaptation measures) za kupambana na climate change ambazo ni kama kuweka irrigation system kwa kutumia water bodies (lakes, rivers, maporomoko ya Maji). Hatuweki km Nchi mipango sawa. Leo tunamsingizia Mungu eti tuombe atupe mvua. Insanity kabsa.! Mwenyezi Mungu ameshatupa akili na maarifa ya kujua how kukabiliana na Mabadiliko ya hali ya hewa.
Leo mwanasiasa km Chiza anatumbia tufunge na tukeshe tuombe mvua ije. Kweli Viwanda vipo karibu. Kilimo kitakufa kwa kusubili mvua. Wazungu wanakimbia kwa maendeleo siye tunarudi nyuma. Najua hatuwezi kutumia ndege/ drones kumwagiliaji Maji but tunaweza tenga maeneo strategic areas kwa kilimo cha umwagiliaji Nchi nzima.
Kufunga na kuomba tutalata vidonda vya tumbo tu..solution tunazo..Mungu ameshatupa maarifa siku nyingi. Kutokutumia maarifa na ujuzi ni kumuudhi Mungu. Mifugo inakufa tunachojua ni kupatanisha tu wakulima na wafugaji kuhusu sehemu ya malisho.
NopeIrrigation system inatengenezwa na serikali mkuu. Ndo maana tunalipa kodi
Watanzania wanapenda sana matukio ya kufuata upepo, kitu kidogo kikitokea wanakikomalia na kusahau vitu vingine vyenye effect za muda mrefu, ukitaka kuwa distract ni rahisi sana, mfano ni ishu ya makonda kutaja watu alioambiwa wanahusika na madawa, basi kwenye jukwaa la siasa kila uzi ni hoja kuhusu madawa ya kulevya basi...Kuombea mvua ni kichekesho kikubwa sanaMkuu bandiko lako lina mantiki sana lakini usishangae kuona watu wanalichukulia poa, hili ni jambo hata mimi huwa linanishangaza siku zote, akili tunazo lakini hatuzitumii, unaweza ukakuta mtu anakaa karibu na mto lakini pembeni mahindi yanakauka eti mtu anasubiri mvua, nakumbuka kijijini kwetu kuna mzee mmoja wakati wa kiangazi aliamua kumwagilia migomba yake, watu wengi walimuona kichaa !!! kisa anamwagilia migomba!
Yaani sisi ni kama tunaishi zama za mawe, wakati wa uchaguzi utasikia eti wanaombea amani, huu ni upuuzi mwingine, amani inakuja kwa kila mtu kutendewa haki, hakuna mtu kichaa anayeweza kuamua kufanya fujo wakati kila kitu kiko wazi, if you conduct free, fair and transparent election it is implicitly that peace will prevail. Wakati wanaombea amani huku wameagiza magari 700 ya washawasha huku wanapita mitaani kutisha watu at the end of the day wanalaumu kwamba wapiga kura ni wachache.
Na wewe tuelekeze huko ambako mvua inanyesha kwa sababu ya maombi ili tuige uombaji wako.Tuelekeze ilipo irrigation system yako tuje tujifunze.