Karibu tuorodheshe mila potofu

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,305
Kila mara "Mila Potofu" hutajwa kwamba ni kikwazo cha maendeleo. Binafsi hupata taabu kuelewa hizo mila potofu.
  1. Mila potofu ni zipi?
  2. Ziliwekwa kwa makusudi gani,
  3. Na nani aliyeziweka,
  4. Kisha ni nani mwenye mamlaka ya kuamua mila hii ni potofu na ile ni sahihi.
  5. Mila potofu ni zipi?
  6. Nini zinafanya ziwe potofu?
  7. Na nini mbadala wake?

Tuziorodheshe hapa.

NOTE TO EDITORS: I appreciate the powers editors have to alter content. But they should put a note to show the changes they have put to a post. Msitulishe maneno. Acheni vilevile tulivyoposti.
 
Mila potofu ni tafsiri tu iliyopewa na jamii ya kuona baadhi ya mila zimepitwa na wakati na ni danganyifu. Mfano kuamini Mzee akiwa na macho mekundu ni mchawi. Au Viungo vya binadamu vinaweza vikakupa utajiri.
 
Mjamzito akila mayai atazaa mtoto asiye na nywele,au mwanamke akila firigisi ataota ndevu,ni uroho tu wa akina baba.
 
Ni utaratibu wa jamii Fulani wa kufanya mambo..kwa mfano baadhi ya makabila mwanamke akifiwa na mumewe lazima arithiwe..
 
Kwamba ukipiga show ukakojoa ndani ya dakika moja ni vibaya na ukipiga show usipige chini ya goli 3, hizi ni imani potofu.
 
Mjamzito akila mayai atazaa mtoto asiye na nywele,au mwanamke akila firigisi ataota ndevu,ni uroho tu wa akina baba.
Hii mila ilikuwa nzuri sana. Ilisaidua akina mama wasife wakati Wa kujifungua maana akila mayai mtoto atakuwa mkubwa hivyo kushindwa kutoka kwa njia ya kawaida. Kumbuka hakukuwa na operations kama Leo.
 
Mila potofu ni nadharia mbali mbali ambazo watu au jamii hujiwejea kwa kulinda maslahi yao
 
Mila potofu iliyovunja rekodi na haifai tuipige vita kabisa ni kulazimisha watu waoneshe vyeti halafu unawaacha mbeleko nibebe wa kolomije.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…