KARIBU MHE BABA MCHUNGAJI PETER MSIGWA CCM.
Na Elius Ndabila
0768239284
Nimeona mjadala mkubwa juu ya ujio wa Mhe Baba Mchungaji Peter Msigwa CCM. Wapo wanaofurahia ujio huo na wapo wanaoponda. Wote wapo sawa. Mimi kabla sijatoa hoja zangu ninaunga mkono ujio wa Mhe Baba Mchungaji Peter Msigwa CCM na nipo tayari kutetea hoja zangu.
Ninamzungumzia Mhe Baba Mchungaji Peter Msigwa ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Iringa kwa miaka Kumi kupitia CHADEMA, amekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Iringa, amekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Kanda ya Nyasa, amekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kwa muda mrefu. Hivyo unapomzungumzia Baba Mchungaji Peter Msigwa unamzungumzia Mwanasiasa anayeijua siasa.
Baba Mchungaji Peter Msigwa ni mwana theorogia na mchambuzi anayesoma. Ni mtu anayeifahamu siasa ya CHADEMA ndani na nje kwani ameshiriki katika haraka zote za CHADEMA.
Baba Mchungaji Peter Msigwa ameondoka CHADEMA kwa sababu ya uchafu wa Chama hicho ambacho kimegubikwa na Rushwa, ulaghai, ghiliba na udanganyifu. Kabla hajaamua kukiahama CHADEMA alikemea Rushwa iliyokubuhu Kwenye Chama hicho hadharani na alikiri kuwa hakuna anayeonyesha dalili ya kuchukua hatua. Alisema CHADEMA hakitendi yale ambayo kinahubiri hadharani. Alisema kadiri muda unavyokwenda Chama hicho kinazidi kuota mizizi ya Rushwa iliyokubuhu. Mchungaji Peter Msigwa ameona asiwe sehemu ya kuudanganya umma na nafasi yake. Ameona CCM ndipo mahali pekee unapoweza kufanya siasa na ukawa salama.
Hata hivyo lengo la Chama chochote cha siasa Duniani ni kushika Dola. Ili Chama kiweze kushika Dola kinatakiwa kushinda Uchaguzi na ili kiweze kushinda Uchaguzi kinahitaji kuwa na watu/Wafuasi. Sera safi na Itikadi safi ya Chama ndiyo inayovutia watu wengi kuwa sehemu ya hicho Chama. Hivyo CCM inahitaji kuendelea kuwa na watu wengi ili kuendelea kubaki madarakani. Mchungaji Peter ni mtu hivyo ujio wake Kwenye Chama ni assert na siyo liability.
Mchungaji Peter Msigwa siyo liability huyu ni mtu mhimu hasa kipindi hiki ambacho nchi inaendelea kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi.
CCM ni Chama Cha Watanzania Wote na wote wanapata fursa sawa.