Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,642
- 6,072
Kuna taarifa zisizokuwa na chembe ya ukweli ambazo zimezushwa na kusambazwa mitandaoni, ikiwa na pamoja na jukwaa hili zikijaribu kumhusisha Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kuwa amechukua zabuni zote katika Wilaya ya Hai.
Haya yote ya kutuhumiwa yamekuja baada ya kutumia njia za CCM kuishinda CCM..na hiki ndio kinyesi kuingia chumbana alivyosema Dr.Slaa,leo hii viongozi chadema wanatuhumiwa ufisadi angali sio watawala.Ajizi nyumba ya njaa!..ni ngumu kuaminika tena na huu mtego ushanasa....Makene sisi tunaojuwa sayansi ya siasa hili ni anguko,pia mwambie Mbowe aache kumshambulia Slaa kwenye gazeti lake!Kuna taarifa zisizokuwa na chembe ya ukweli ambazo zimezushwa na kusambazwa mitandaoni, ikiwa na pamoja na jukwaa hili zikijaribu kumhusisha Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kuwa amechukua zabuni zote katika Wilaya ya Hai.
Wanaosambaza uongo huo, wamesema kuwa Mwenyekiti Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amefanya hivyo kwa ubabe.
Ni vyema tukaweka ukweli kuhusu uzushi huo ambao umeanza kuwasumbua wanachama, wapenzi, mashabiki na wapenda mabadiliko kwa ujumla, kuwa Mwenyekiti Mbowe hana zabuni yoyote katika Wilaya ya Hai wala hajawahi na hana zabuni katika wilaya yoyote nyingine katika maisha yake yote ya uongozi na utumishi anaowajibika kwa umma.
Halmashauri ya Wilaya ya Hai kama yalivyo maeneo mengine ya halmashauri, manispaa na majiji ambayo yako chini ya uongozi wa Chadema na UKAWA kwa ujumla inajiandaa kuwa mojawapo ya maeneo ya kupigiwa mfano kwa mabadiliko yatakayofanyika kutokana na kusimamia uwajibikaji utakaotanguliza uadilifu mbele wenye dira ya maendeleo kwa ajili ya wananchi.
Hai ni halmashauri ambayo tayari imeweka rekodi kadhaa, kwanza inaongozwa na CHADEMA kwa 'full majority' kwa maana ya madiwani wanaounda baraza ambalo liko chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri mwanamke ikiwa ni mara ya kwanza.
Makene
Halafu nimeambiwa wewe mbali ya kuwa umo kwenye "List of 46" kumbe pia taaluma yako ni ualimu, Aibu ilioje!!Gazeti la kuaminika la habari za uchunguzi la JAMHURI wafuatilie watuambie ni kweli au si kweli
Sasa hivi ni full kujitetea!Mbowe naye fisadi tu...
Kabla ya Lowassa kujiunga na CHADEMA Mbowe aliwahi kutuhumiwa na wajinga hawa hawa kwamba "ameifilisi" NSSF. Kama unataka kusema Slaa asishambuliwe anzisha uzi wako kuhusu huyo Mla mihogo na Mchumba wake!!Haya yote ya kutuhumiwa yamekuja baada ya kutumia njia za CCM kuishinda CCM..
Kijana Allen,kinyesi kimehamia kitandani...maneno ya Dr.Slaa yanatimia...yaani leo hujatawala nchi anatuhumiwa ufisadi...dah siku zinaenda kasi.Ngoja tupate ripoti ya Monduli,Kinondoni nk...japo Monduli EL ni shamba lake!Halafu nimeambiwa wewe mbali ya kuwa umo kwenye "List of 46" kumbe pia taaluma yako ni ualimu, Aibu ilioje!!
"Ukiamishia kinyesi kitandani lazima chumba kinuke"..Dr.Slaa 1.9.2015Mkuu hapo ume-act kama msemaji wa chama au wa Mbowe?
Nakumbuka hata ile ya kuhamisha mabilioni ya fedha uliitolea tamko (kama sijakosea).
Kuna thread zako mbili naziweka hapo chini zinazoniambia wewe ni kanjanja tu kama makanjanja wengine, unatumika tu kama wanavyotumika wengine.
Zitto amemtuma ofisa wake kuisemea CHADEMA kuhusu Lowassa!
Kama ni kuhusu akina Lowassa na CCM yao, M/kiti Mbowe amesema
Unaposema "naye fisadi" Unamlinganisha na Mkapa aliyejiuzia Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira. Au unamfananisha na yule aliyepewa Gawiwo la dili la Rada na Escrow? Au yule mwenye mahusiano na Home Shopping Center? Mbowe Hafanani na hao wote hata kwa harufu tu!Mbowe naye fisadi tu...
Shika adabu yako na adabu ikushikeKijana Allen