Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 26,081
- 62,748
KANUNI ZA KUOMBA MIUNGU NA KUJIBIWA
Anaandika, Robert Heriel,
Kuhani Katika Hekalu Jeusi,
Mtibeli.
Watu wengi wanauliza swali hili. Wengine wananipigia simu wakitaka kujua wafanyaje ili maombi Yao kwa Mungu yajibiwe.
Mimi kama Taikon Master, Kuhani Katika Hekalu Jeusi. Niliye na uzoefu katika mambo hayo nikasema nitatoa dondoo chache zitakazo kusaidia kuomba kwa usahihi na kujibiwa kwa wakati.
Zifuatazo ni mbinu za kuomba maombi kwa Mungu kisha ujibiwe kwa Wakati;
1. Mbinu ya kuwa Kimya, mtulivu,
angalau kwa masaa kadhaa au siku kulingana na jambo unalotaka kuliomba.
Sio unatoka kibaokata, au unatoka Bar, au unatoka kazini, au unakurupuka tuu unasema unaenda kuomba. Nope!
Maombi ni mawasiliano ya nafsi ya mtu na MIUNGU.
Huwezi kuomba miungu kwenye makelele, kwa makelele au nafsi yako ikiwa na makelele.
a) kwa Makelele!
Huwezi mwomba mungu kwa Makelele kama kichaa. Kupiga Makelele, kuongea ongea Maneno yasiyopangilika na yenye heshima ni dalili ya kuchanganyikiwa.
b) kwenye Makelele.
Huwezi kuomba Mungu sehemu yenye Makelele.
Kelele ni kiashiria hakuna nidhamu. Hakuna heshima.
Hata hapa duniani sehemu zenye kelele huwa za wahuni, watu ambao sio waungwana.
Maombi yanahitaji sehemu iliyotulia.
C) nafsi ikiwa na Makelele.
Kuna mbinu ya kutuliza akili na nafsi ifikirie Jambo Moja. Yaani kudhibiti mkondo wa mawazo na kuwaza kile unachotaka.
Huwezi kuwa unawasiliana na Mungu alafu katikati ya mawasiliano kunaingia mawazo(mawasiliano )mengine. Ni kama meter band za radio. Una switch meter band ya redio Fulani alafu zinaingiliana na redio nyingine.
Unaomba alafu katikati ya maombi unashangaa unawaza Vikoba, au mara paap unawaza mkeka uliobet. Au unamuwaza Pacome, hapo hakuna unachofanya.
Maombi hasa maombi maalumu yanahitaji udhibiti wa mawazo na hisia zako.
Mbinu Mojawapo ya kuyatuliza mawazo yaende kwenye mkondo unaoutaka;
I) Oga ujitakase mwili wote.
ii). Tafuta nguo nyepesi zisizokubana yaani zinazoruhusu mzunguko wa damu utembee. Wengi hapa wanavaa Majoho, Kanzu, kaniki, .
iii) Tega Muda katikati ya siku.
Mfano katikati ya mchana na usiku.
Usiku na asubuhi, asubuhi na mchana.
Hapo akili inakuwa inasizi na inakuwa kama na uchovu. Nazungumzia saa tano asubuhi Mpaka saa sita unusu mchana.
Saa tisa unusu na saa kumi jioni.
Au saa tisa usiku kwenda saa kumi. Ambapo usiku na alfajiri hutengana.
Kama utashindwa kabisa fuata kuwika kwa jogoo mwenye umri Mkubwa. Akiwika unaweza kujiandaa kwa maombi
Iv) lala chali angalia juu fumba macho kisha isikilizie pumzi unayovuta puani. Kwa dakika tano mpaka kumi. Hakikisha usijepitiwa na usingizi.
Hii utafanya kama ndio Kwanza unaanza.
Hii inaenda sambamba na kuketi na kukalia miguu kama unafanya tahajudi
v) Au kaa mbele yako uwepo mshumaa kisha utazame mshumaa unaowakaa kwa dakika tano mpaka kumi. Kisha fumba macho. Kaa tena dakika tano kisha anza kuomba Hakikisha pumzi inayoingia na kutoka puani unaisikia usijepitiwa na usingizi.
Kama utakuwa mtu wa keto nyingi, masumbuko Mengi, hangovers, pombe, na mtu mwenye shutuma nyingi.
Zamisha kichwa kwenye maji kwa sekunde 40-60 kwa anayeanza.
2. Mbinu ya Pili, Maombi ya Shukrani na kujitakasa.
Usiwe ombaomba kwenye Maombi yako. Kuomba omba wakati mwingine ni dalili ya kukosa Shukrani.
Jitahidi kila uombaji Shukrani ziwe nyingi kuliko Maombi ya shida zako.
Kushukuru ni kuonyesha umeweza kutumia kile ulichopewa. Kuwaza kutumia kile ulichopewa inamaanisha ni useful na baraka.
Huwezi kuomba vitu vingine wakati vile ulivyopewa umeshindwa kuvitumia.
Kushukuru ni sehemu ya kujitakasa na kuomba toba kwa baadhi ya makosa uliyoyafanya Kwa baraka ulizopewa.
Kadiri unavyoshukuru ndivyo unavyozidi kubarikiwa
Namna ya kushukuru;
I) kutumia kwa usahihi kile ulichobarikiwa.
Mfano, unasauti nzuri, ukaitumia kuhubiri na kuwafundisha watu wakaelimika. Huko ni kuonyesha Shukrani
Unajua kuimba, unaimba nyimbo watu wanaburudika, wanaelimika, wanaonyeka, huko ni kushukuru MUNGU.
Unaelimu Fulani unawapa watu, wewe ni Mwalimu au Mwanasheria au Daktari au dereva vile unavyofanya Kazi na watu wakaifurahia Kazi yako huko ndiko kunaitwa kushukuru.
ii) Kusaidia wengine bure(kutoa Sadaka) kwa wahitaji.
Hii ni kubwa kuliko.
Kwenye Kazi zako lazima uhakikishe asilimia kadhaa zisizopungua asilimia kumi unawasaidia watu wenye uhitaji.
Mfano, wewe ni Daktari unaweza ukapanga kwenye wateja kumi Mmoja utamsaidia bure hasa wenye Hali ya uhitaji, umaskini.
Au Mwanasheria, kwenye wateja kumi Mmoja nitamsaidia bure kama Sadaka.
Kumshukuru Mungu tafsiri yake ni watu kuona Tija yako. Yaani watu wengine kumshukuru Mungu kupitia maisha yako.
Sio wewe kwenda MWENYEWE kumshukuru Mungu kwa mdomo pekee.
Kadiri unavyoshukuriwa ndivyo kadiri Mungu atakavyokuinua. Hiyo ni KANUNI.
iii) Msamaha
Kutoa Msamaha ni sehemu ya kumshukuru Mungu na kujitakasa.
Msamehe anayehitaji Msamaha kwa dhati.
Msamehe ambaye amefanya Jambo bila dhamiri/kusudi.
3. Mbinu ya Tatu,
Lazima Maombi yawe Ofisho/Rasmi.
Lazima upange Muda na namna ya maombi yako yatakavyofanyika.
Sio kuomba kama mhuni na kihuni. Yaani ukiwa na shida ndio unaomba.
Ni Sawa upo na ndugu alafu anakutafuta Akiwa na shida. Huo ni Uhuni na dharau. Dalili ya kutothamini. Kuwa after something.
Maombi lazima yawe Ofisho. Kwamba kila siku naomba Mara mbili au mara tatu, saa Fulani, Fulani na Fulani. Jumanne na ijumaa nafunga.
Kila mwezi wa kumi natoa chakula kwa wahitaji. Kila baada ya miezi miwili nafanya matendo ya huruma. N.k.
Hiyo inaitwa nidhamu na heshima.
4. Wakati unaomba usiwe tayari unajua mbinu ya kufanikisha Jambo Fulani unaloliomba. Yaani namna itakavyokuwa.
Omba ukiwa hujui itakuwaje.
Mfano, hujui utapataje gari lakini omba Kupata gari.
Jambo lolote ambalo unaliomba ukiwa na njia possibility ya Jambo hilo kufanikiwa ni ndogo.
Maombi ni kwaajili ya mambo yasiyowezekana.
Usiombe ombe vitu vilivyo ndani ya uwezo wako. Hiyo kiprotocols ni ukosefu wa nidhamu.
5. Heshimu Njia unayoipita, uliyopo. Usiidharau.
Maombi hayafanyi Kazi kwa njia ambayo haupo.
Sehemu uliyopo ndio sehemu sahihi kwa maombi yako kujibiwa.
Mfano, usidharau Kazi unayoifanya hata kama inakipato DUNI ukaona haitakufikisha sehemu uliyomuomba Mungu.
Kitendo cha kuona hustahili kuwa Njia hiyo ndivyo ambavyo huwezi kutoka hapo.
Tumia Njia uliyopo kwenda Njia unayo ihitaji. Tumia ulichonacho Kupata kile unachoomba Mungu. Hiyo ni KANUNI
Kwa Lugha nyingine usiwe mlalamikaji.
Mfano, wakati wengine wakiona hakuna ajira, tumia kutokuwa na ajira Kupata ajira. Lakini kadiri unavyosema hakuna ajira alafu unaomba Mungu akupe ajira ndivyo macho yako hayataona ajira na hutafanya lolote.
Unapambana na adui, upo vitani. Badala ya kulalamika adui amekuzidi uwezo na ukubwa tumia mbinu nyingine za kivita hata kukimbia ili Mungu akujibu Maombi yako.
Wakati wengine wanaona ndoa na mahusiano ni utapeli na kuna upigaji. Usiwe miongoni mwao. Macho yako yaone Wema ili Mema yakujie. Kadiri unavyoona wema hata kama ni mdogo kama mchanga ndivyo Mema makubwa yanapokujia.
Wakati wengine wanaona hakuna Pesa wewe usione hivyo. Hata kama pesa unayoiona ni cent Moja ona IPO pesa nyingi.
Hizo ni KANUNI ZA watibeli wote.
Unapomwomba Mungu elewa unaomba ushindi. Na ukiomba ushindi elewa unaomba kushinda. Hivyo lazima macho yako yaone kila kitu katika ushindi, yasikie ushindi, yatafakari ushindi, yatafute Njia ya ushindi na ushindi utakujia.
Watibeli siku zote hushinda popote na kwa yeyote.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam