Kamusi ya majina ya samaki na picha zao

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,467
158,081
Majina ya Samaki , Maelezo na Picha (SAMAKIPEDIA)

Blobfish
images (7).jpeg

Blobfish ni samaki anayetajwa kwamba ni kiumbe mwenye sura mbaya na muonekano usio vutia kuliko kiumbe chochote.
FB_IMG_16045658861920659.jpg


Blobfish Ni samaki wa kawaida anayepatikana kwenye kina kirefu Sana cha bahari kati ya futi 2,000 hadi 4,000.
Presha ya huko inamfanya awe samaki wa kawaida kabisa na akiwa kwenye makazi yake huko chini anakuwa na sura kama ya samaki wengine wa kawaida. Lakini anapodakwa na nyavu za wavuvi wa kina kirefu na kufikishwa huku juu presha hubadilika na hivyo kumfanya apoteze sura yake asilia. Samaki hawa hupatikana zaidi New Zealand, Australia na Samoa.


Bunju
Samaki aina ya Bunju wapo wa aina mbalimbali. Wapo wenye ngozi yenye miiba.
bunju-miba wana sumu inayoitwa tetrodotoksini, inayopatikana zaidi katika maini, mifuko ya mayai, figo, na wakati mwingine kwenye ngozi ya samaki huyo. wapo wasio na miba pia wapo wenye sumu Kali Sana.




Chaa (Common Silver Biddy)
Chaa_Humphreys_Seafood_Distributors_Bujibuji.JPEG


Changu Batu/ Mjibondo/ Kitawa ( Big eye Emperor)

kwa Kingereza Bigeye Emperor (Monotaxis grandoculis, Mū in Hawaiian) ni Samaki asiye wa kawaida, kama ng'ombe wa mwamba wa majini kwa namna wanavyoishi kwa kujikusanya kwa makundi na kujivinjari majini.
Wana namna yao ya kipekee na kistaajabisha, wanakuwa kana kwamba wameganda, Kama hawatembei. Ukijaribu kuwasogelea kimiujiza huwepo Tena mbali na wewe wakiwa wameganda Tena na kuendelea kushangaa.
Samaki hawa hupendelea kula kaa na viumbe wadogo wa baharini hasa kwenye miamba.
Samaki hawa wanna meno yaliyofanana na magego kwa ajili ya kutafunia na kusagia magamba ya kaa na konokono, na meno yao ya mbele Yana ncha kali kwa ajili ya kukamatia kitoweo.
Changu Batu hupatikana kwenye bahari ya Hindi na Pacific na usiku ndio muda ambao huupenda zaidi kuutumia kuwinda


Changu Chali (Blubberlip Snapper)

Changu Chali kwa Kingereza Blubberlip Snapper, na kwa jila lake kisayansi anaitwa Lutjanus rivulatus, also pia hujulikana kwa jina la Maori Snapper, ni aina ya Changu mwenyeji mkaazi wa Bahari ya Hindi na pia hupatikana katika Bahari ya Pacific.
Samaki hawa hupendelea kukaa kwenye majabali ya baharini, kwenye mapango bahari na kwenye matumbawe.
Hupendelea zaidi kuishi kwenye kina Kati ya mita 15 Hadi mita100 (49 to 328 ft).
Urefu wake ni hufika hadi 80.0 cm au inch 31.5 .
Pia uzito wao hufika hadi 13.0 kg (28.7 lb).
Samaki hawa hupendelea kutembea wachache, Kati ya mmoja mmoja au kwenye kundi lisilozidi samaki 20

Changu_Chali_(Blubberlip Snapper)_Bujibuji.JPEG



Changu Doa/ Mkapa/ Kiwala (Thumbprint Emperor)
Jina lake la Kibaiolojia ni Lethrinus harak, almaarufu kwa Kingereza kama The Thumbprint Emperor au Waingereza wengine humuita Blackspot Emperor.
Samaki huyu ana rangi ya mchanganyoko wa zaitu na kijani, na upande wa tumboni ana mpauko.
Changu Doa hufika hadi urefu wa 50 cm ila wengi huvuliwa wakiwa na urefu wa 30 cm. Jina la la Changu Doa linatokana na baka kubwa jeusi walilonalo kwenye pande zao zote mbili.
Baka hili mara nyingi huzungukwa na rangi ya njano.

Mara chache huwa na mabaka ya bluu yaliyopauka maendeo yao ya puaniThere are occasionally pale blue dots na maeneo yanayozunguka macho.
Mapezi yake huwa na rangi ya machungwa na wakati mwingine nyekundu.
Changudoa_Thumbprint Emperor_Bujibuji.JPEG



Changu Mwekundu (Red Snapper)
RED-F.jpeg



Changu Chana

Chaza (Oyster)

Chewa

Samaki huyu ni aina ya chewa hupatikana bahari ya Hindi hasa hasa pwani ya Afrika Mashariki. samaki huyu akiwa na ukubwa wakawaida huparuliwa magamba lakini kwa walio kuwa wakubwa sana huchunwa gamba la nje na kupatikana mnofu (fillet).
Samaki huyu ni mtamu sana kwa supu.
Chewa huwa na rangi ya kahawia na madoa meusi.
Ana mdomo mkubwa na samaki huyu hafi kirahisi.
Anaweza kukaa masaa zaidi ya sita akiwa hai, hata kama ni mdogo.
Samaki huyu hata akitolewa utumbo wake na vitu vya ndani huendelea kupumua.
Chewa_Grouper_Humphreys_Seafood_Distributors_Bujibuji.JPEG



Dagaa (Sardines)

Hawa ni samaki wadogo ambao pia hupewa majina mengine mengi kama kauzu, misumari nk.
Dagaa ni watamu Sana hasa wakipata mtu anayejua kuwaunga vizuri, na wanafaa zaidi kuliwa na ugali
Dagaa_Humphreys_Seafood_Distributors_Bujibuji.JPEG

Dome (Cuttlefish)
tumblr_mv6oluvcO21qm9k25o3_1280%20(1).jpg

Dome Ni samaki jamii ya ngisi mwenye gamba gumu ndani mgongoni. Kama jamii nyingine za ngisi, dome ana wino na ana sumu kwa ajili ya kujikinga na maadui zake. Dome hashambulii binadamu.

Domodomo
IMG_20201105_065635.jpg

Domodomo Ni samaki anayepatikana katika maziwa yote makubwa hapa nchini Victoria, Nyasa na Tanganyika na amekuwa akijulikana kwa majina mbalimbali kama Ndomolomo (Kigoma), Njizi (Nyasa) na Mbete.

Furu (Haplochromis) Chichlids.
download (5).jpeg
download (4).jpeg

Furu ni samaki anayepatikana ziwa Victoria, ambaye anakuwa Hadi kufioia urefu wa sentimeta 25. Wana Tundu moja la pua kwenye Kila upande. Samaki huyu msogomdogo, Ni maarufu Sana na anapatikana kirahisi.

Gaegae(Solefish)
Jodari
Joza
Kamba
Kamba Kochi
Kamongo
Kamongo%2B1.jpg

Samaki aina ya Kamongo...



Samaki hawa wanaumbo kama la nyoka...samaki hawa hawafi haraka hivyo anavyoonekana hajafa lakini unaweza kudhani kafa.Ukimshika unatakiwa uwe makini usimpelekee kidole kinywani anauwezo wa kuking'ata chote.

Hata akikatwa vipande bado mapande yake yanakuwa yana uhai yanajikunja hivi kila ukiyapiga mpaka mshipa fulani hivi utolewe kwenye uti wake wa mgongo.

Kwa sababu ya ngozi yake kufanana na nyoka hivyo waandaaji na wauzaji wa samaki huyu huwalazimu kumkata minofu tu na kuitupa ngozi yake.Ni samaki mtamu
Kapungu ( Shark)

Karambisi

Kelea


Kibua Mackerel Fish
1604778241048.png
Samaki aina ya kibua wamegawanyika wa aina kadha wa kadha. Wapo kibua wenye mwamba mgumu kwenye ngozi zao, mwamba huo mgumu huanzia mkiani hasi maeneo jirani na tumboni.
Pia wapo vibua wenye ngozi laini isiyo na ugumu wowote. Vibua wote ni watamu sana na bei yake haitishi, ni bei rafiki.


Kolekole
IMG_20201018_152959_299.jpg


Mbofu (Bagrus meridionalis) Catfish
800px-Catfish_in_Lake_Malawi.jpg

Mbofu Ni samaki jamii ya kambale, anayepatikana Africa tu. Samaki huyu huweza kufikia urefu wa mpaka mita 1.5 na anapatikana ziwani, hasa ziwa Victoria na ziwa Nyasa licha ya kwamba Sasa wanapatikana kwa uchache kutokana na sababu mbalimbali.


Migebuka Lates stappersii, The Sleek lates
images (8).jpeg
Migebuka ni samaki ambaye duniani kote anapatikana katika ziwa Tanganyika pekee. Urefu wake hufikia hadi sentimeta 45.
Migebuka Ni watamu sana lakini upatikanaji wake ni mgumu kutokana na urefu wa kina cha ziwa Tanganyika na zana duni za uvuvi.


Mkunga umeme (Electric eels)
Duniani yapo mengi ambayo yanavuta hisia ukiyasikia. Wengi wetu huamini kuwa umeme umekuwa ukizalishwa kutoka katika vyanzo mbalimbali kama mashine, betri, jua na maji.

Lakini amini au usiamini kuna viumbe ambao wanazalisha umeme mwingi wenye nguvu hata ya kuweza kumuua binadam mtu mzima ndani ya sekunde...lakini pia hata MAMBA HAFUI DAFU kwa samaki huyu achilia binadamu

Moja ya viumbe wenye uwezo wa kuzalisha umeme ni samaki aina ya electric eel au electricus fish ambae ana umbo refu mfano wa bomba huwa akikuwa anaweza akafikia urefu wa mita 2 ( futi 6-7) na uzito wa kilo 20 kitu kinachomfanya kuwa samaki mkubwa katika kundi la Gymnotiformes.

Electric-Eel.jpg
Katika samaki anayeogopeka na kumshika kwake lazima uwe makini huyo electric fish. wanakuambia hata aikwa nje ya mtumbwi anauwezo wa kutoa umeme wa kutosha kukuumiza sentimita chache kutoka alipo....NASIKIA HAPA Tanzania pia wapo (ila sio Kamongo)

Electric eel ana viungo tofauti vinavyomsaidia kuzalisha umeme, cha kwanza kinazlisha umeme kwa ajili ya kuwindia na kingine kinazalisha kwa ajili kusikilizia.

Viungo hivi vya kuzalishia umeme vinatengeneza 4/5 ya mwili wake wote, na vinmuwezesha kuzalisha umeme wa aina mbili ule wenye nguvu kubwa na ule wa nguvu ndogo. Viungo hivi ambavyo vimeundwa na elektroliti vimejipanga kwa pamoja ambapo ngunvu ya umeme inapita kama vile ufanyavyo kwenye waya.

Kipindi eel anapohisi windo ubongo wake hutuma taarifa kwenye elektroliti na hii hupelekea kufungua chaneli ya madini yachuma ambayo inaruhusu sodium kupita kwa kubadili mkondo kurudi nyuma ambapo mabadiliko ya haraka hutokea katika mkondo na kupelekea kuzalisha umeme kama vile betri ambapo seli hupangwa pamoja ili kupata umeme.
maxresdefault.jpg
Ndani ya electric eel, baadhi ya seli 5,000 mpaka 6,000 zilizojipannga kwa pamoja ambazo zina uwezo wa kuzalisha volt 860 na watt 860 ndani ya chini ya sekunde moja. Umeme huu una uwezo wa kumdhuru hata kumuua mtu mzima.

Pia ndani ya smaki huyu kuna ogani nyingine ijulikanyo kama Sach’s ambayo inaundwa na seli nyingi ambapo kila seli inazalisha umeme mdogo wa volti 0.5, organi hii inazalisha umemewa 10V katika mawimbi ya 25hHz kwenda juu , ambapo huutumia umeme huu mdogo kwa ajili ya kufanya mawindo yake hasa ukizingatia kuwa hana macho.

Pindi samaki huyu anapojihakikishia kuwa windo lake lipo ndani ya mzio wake basi huachia ule umeme mkubwa ambapo ukimpata windo basi hupoteza nguvu na hivyo kumezwa na samaki huyu.

Electric eels amekuwa akifanyiwa uchunguzi wa bioelectrogenesis. Na amekuwa ni kivutio kwa watafiti, ambapo watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani na wizara ya taifa ya teknolojia wanajalibu kuona kama wanaweza kutengeneza seli feki zinazofanana na za samaki huyu au kuboresha seli za samaki huyu. Uzalishaji ama uboreshaji wa seli hizo unaweza kuendelezwa kisayansi ili kuweza kuwa kama chanzo cha nguvu kwa viungo vya vya bandia na vifaa tiba.

Electric eels anaishi katika maji ya baridi(yasiokuwa na chumvi) katika msitu wa Amazon na katika bonde la mtoOrinoco huko America kusini. Na maranyingi hupatikana katika kina cha mto katika maji yaliyotulia kiasi.

Chakula chake kikubwa ni wadudu, konokono, kaa, minyoo ingawa mala nyingine anaweza kula samaki na wanyama wadogo wadogo kama panya.

Uzalialianaji wake ni wa kutaga mayai kipindi cha kiangazi ambapo hutaga mayai karibia 3000. Samaki jike ndio mwenye umbo dogo kuliko dume.



Mtepa Ribbon Fish
images (9).jpeg

Mtepa pia anajulikana kwa majina yake mengine ya Kingereza kama The largehead hairtail au beltfish.
Samaki huyu analadha nzuri sana ukimkaanga. Anafaa kuliwa na chips au mihogo kama kifungua kinywa na chai


Nembe
IMG_20201105_061741.jpg

Nembe Ni samaki wa maji baridi na anapatikana Sana ziwa Victoria, hasa mvua zinaponyesha.
Samaki Nembe ni mtamu hasa kwa chukuchuku,ukimuosha vizuri mchemshe kidogo na umkatie nyanya na kitunguu humohumo bila kusahau limao na chumvi ni mtamu sana.Samaki huyu analiwa na mayai yake ukimsafisha usimtoe mayai.

Ngisi
IMG_20201014_224105_471.jpg
FB_IMG_16009165655566834.jpg



Ningu

Nyangumi

Nyangumi ni wanyama wa bahari, na pengine wa maji matamu, wanaofanana na samaki, lakini ni mamalia: kwa hivyo hawatagi mayai kama samaki bali huzaa watoto kama mamalia wote na huwanyonyesha.

Pamoja na nguva, wanyama hawa ni mamalia pekee wanaoishi kwenye maji tu.
Pandu

Pono

Pweza ( Octopus)
FB_IMG_16047876358910551.jpg

Pweza ni kiumbe wa baharini mwenye macho, kichwa, mdomo na mikono nane. Kiumbe huyu mjanja na mwerevu hukaa kwenye majabili, kwenye sakafu ya bahari na mapango ya bahari ana uwezo mkubwa sana wa kuwadhibiti na kuwatoroka maadui zake inapotokea hatari.
Miongoni mwa mbinu zake ni pamoja na kujibadilisha rangi, kutifua maji wino wake na kutoroka, na akishindwa kabisa hutumia mikono yake nane yenye nguvu kumdhibito adui.
Ulaji wa pweza una faida nyingi sana kwa afya ya uzazi.
(Pweza wa kukaangwa)

Sangara

Sapalala
1604779577664.png

Sapalala ni viumbe wa baharini ambao wamefanana kwa namna fulani na kamba. Sapalala sio maarufu sana kwa soko la ndani ya nchi kwani Waswahili hatuwapendi na hatuna mwamko wa kuwaonja, ila wenzetu wa Asia ya Mbali China, Korea na Japan, wanawapenda sana na huwanunua kwa wingi.


Sato


Sesemvule (Stonefish) scientific name

Synanceia​

Synanceia_verrucosa_Hennig.jpg

Sesemvule ni samaki anayekaa kwenye sakafu ya bahari na ana rangi na muonekano wa mawe ama miamba ya baharini.
Samaki huyu ambaye sehemu kubwa ya mwili wake imefunikwa na Miiba mirefu hivyo kumfanya asionekane kirahisi pindi awindapo

Songoro


Tasi, rabbit fish (Siganus sutor)
IMG_20201008_091806_4.jpg

FB_IMG_16009989742992308.jpg

Tasi Ni samaki mtamu sana anayekula majani. Tasi hudakwa kwa mtego ujulikanao kwa jina la dungu. Tasi ana miiba mikali Sana ambayo ikikuchoma hukuachia maumivu makali sana. Mwiba wake uliopo kwenye paji la uso ambao hueleke mbele mdomo uliko Ni hatari Sana, una maumivu atakayokufanya ukae chini na kuvimba wiki nzima. Mshike kwa tahadhari kubwa hata akiwa amekufa


Tasi Mwamba
FB_IMG_16008045921650172.jpg

FB_IMG_16009990953795440.jpg

Tasi mwamba ni jamii ya tasi ambayo ina magamba na hupatikanika kwenye majabali chini ya bahari.

Uduvi Shrimps Alaskan Pink Shrimps
images (11).jpeg

Hawa ni wadudu wadogo wa baharini wenye ladha tamu. Ni jamii ya kamba lakini hawa ni wadogo zaidi.
 

Attachments

  • 34984621_232526724193734_701668454960201728_n.jpg
    34984621_232526724193734_701668454960201728_n.jpg
    55 KB · Views: 154
  • download (5).jpeg
    download (5).jpeg
    7.7 KB · Views: 174
  • images (5).jpeg
    images (5).jpeg
    8.5 KB · Views: 196
Jina la SamakiPicha
Bunju
Samaki aina ya Bunju wapo wa aina mbalimbali. Wapo wenye miiba, wapo wasio na miba pia wapo wenye sumu Kali Sana.



Chaa (Common Silver Biddy)
View attachment 1580605

Changu Batu/ Mjibondo/ Kitawa ( Big eye Emperor)

Changu Chali
(Blubberlip Snapper)View attachment 1580517

Changu Doa/ Mkapa/ Kiwala (Thumbprint Emperor)


Changu Mwekundu (Red Snapper)View attachment 1580516


Changu Chana

Chaza (Oyster)

Chewa

Samaki huyu ni aina ya chewa hupatikana bahari ya Hindi hasa hasa pwani ya Afrika Mashariki. samaki huyu akiwa na ukubwa wakawaida huparuliwa magamba lakini kwa walio kuwa wakubwa sana huchunwa gamba la nje na kupatikana mnofu (fillet).
Samaki huyu ni mtamu sana kwa supu.
Chewa huwa na rangi ya kahawia na madoa meusi.
Ana mdomo mkubwa na samaki huyu hafi kirahisi.
Anaweza kukaa masaa zaidi ya sita akiwa hai, hata kama ni mdogo.
Samaki huyu hata akitolewa utumbo wake na vitu vya ndani huendelea kupumua.
View attachment 1580633


Dagaa (Sardines)

Hawa ni samaki wadogo ambao pia hupewa majina mengine mengi kama kauzu, misumari nk.
Dagaa ni watamu Sana hasa wakipata mtu anayejua kuwaunga vizuri, na wanafaa zaidi kuliwa na ugali
View attachment 1580699
Gaegae (Solefish)
Jodari
Joza
Kamba
Kamba Kochi
Kapungu ( Shark)

Karambisi

Kelea
Kolekole

Nyangumi

Pandu

Pono

Pweza

View attachment 1580495View attachment 1580516View attachment 1580517View attachment 1580605View attachment 1580633View attachment 1580699


Gaegae ( Solefish)



View attachment 1580495
Uzi mzuri sana ila umekosa mpangilio mzuri na ubunifu. Hizi picha zinapatikana mtandaoni kwa nini umetuwekea mapicha yasiyoeleweka.

Tafadhali angalia namna ya kuupanga vizuri ujumbe wako ni moja kati ya nyuzi nzuri sana usiuache upotee kwa maujinga na maharaka yako.
 
Uzi mzuri sana ila umekosa mpangilio mzuri na ubunifu. Hizi picha zinapatikana mtandaoni kwa nini umetuwekea mapicha yasiyoeleweka.

Tafadhali angalia namna ya kuupanga vizuri ujumbe wako ni moja kati ya nyuzi nzuri sana usiuache upotee kwa maujinga na maharaka yako.
Usinifundishe Cha kufanya, buni uzi wako, fanya yako.
Huu uzi ni Mimi ninayeuandaa, na ninajua utaishaje.
JamiiForums haina draft.
Siwazi kuacha kazi zangu za thamani ili nipoteze muda wangu adhimu kukufurahisha wewe.
Ninaendelea ku compose uzi wangu taratibu vibayavibaya na utaisha UKIWA mzuri.
Ni Kama lami, haijengwi kwa siku moja na uvumile diversions zenye mashimo na makorongo, pia uvumilie foleni na vimbi, lami inakuja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom