Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 116
- 204
Wakati wa Mkutano wa Kilele wa Mwaka 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing, Kampuni ya Teknolojia ya Baifenbi ya China ilisaini makubaliano na Wizara ya Posta, Mawasiliano ya Simu na Dijitali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kulingana na makubaliano hayo, pande hizo mbili zitajaribu kujenga mfumo wa usimamizi wa dharura na mfumo wa vitambulisho vya kielektroniki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kutumia teknolojia za kidigitali ili kuboresha kiwango cha usimamizi wa mambo mbalimbali.
Hii si mara ya kwanza kwa Kampuni ya Baifeibi kushirikiana na nchi za Afrika. Mwaka 2017, kampuni hiyo ilishiriki katika ujenzi wa mfumo wa akili bandia wa sera ya idadi ya watu nchini Angola. Hadi sasa, Kampuni ya Baifenbi imetekeleza zaidi ya miradi 10 ya ngazi ya kitaifa katika nchi 4 za Afrika, ikitoa majukwaa ya kitaifa ya data kubwa na akili bandia, pamoja na matumizi ya teknolojia za kidijitali katika mambo ya kiserikali.
Katika miaka ya hivi karibuni, kampuni nyingi za teknolojia za China zimeanzisha ushirikiano na nchi za Afrika. Si kama tu zimeleta teknolojia mpya na vifaa vipya vinavyowezesha matumizi ya vifaa vya kidijitali barani Afrika, bali pia zimeleta seti kamili ya “suluhisho za Kichina” katika kuharakisha kuanza kwa “zama ya kidijitali” barani humo.
Mwezi Mei mwaka huu, Kampuni ya Huawei ya China ilitangaza uzinduzi rasmi wa Kituo cha Huawei Cloud huko Cairo, mji mkuu wa Misri, na kutoa zaidi ya aina 200 za huduma, ikiwa ni pamoja na majukwaa ya AI, na data kubwa. Baadaye kampuni hiyo pia inapanga kuleta teknolojia nyingine mpya zikiwemo modeli ya akili bandia, modeli ya lugha kubwa ya Kiarabu, na mfumo wa kanzidata kwa Misri.
Mbali na miradi hiyo ya “hali ya juu”, kampuni za China pia zinazingatia ngazi ya mashina ili kuwasaidia watu wa kawaida barani Afrika kunufaika na teknolojia za kisasa.
Hivi sasa, nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na haliduni ya miundombinu, watu wengi bado wanatumia mtandao wa 2G wa mawasiliano ya habari, na hata baadhi ya watu wanakosa huduma ya umeme. Katika miaka ya hivi karibuni, Kampuni ya Zhongteng ya China imejenga au inajenga miradi 22 ya umeme ya nishati mpya katika nchi mbalimbali barani Afrika, zikwemo Niger, Ethiopia, Nigeria, na Tanzania, na kuboresha kwa kiasi kikubwa kiwango cha upatikanaji wa umeme katika vijiji vya mbali, na kunufaisha zaidi ya watu milioni 30. Kampuni ya ZTE ya China imesaidia Misri kuongeza kasi ya mtandao kwa zaidi ya mara kumi, na kuwawezesha idadi kubwa ya Wamisri kutumia mtandao wa kasi ya juu.