Kampuni ya Premier Betting yakubali kujenga viwanja vya Kikapu nchini Tanzania

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,669
8,270
Kampuni ya Premier Betting yakubali kujenga viwanja vya Kikapu nchini Tanzania.

Makubaliano hayo yalifikiwa katika kikao kilichowasisha Ndg. Sami Matar Mkurugenzi wa kampuni ya Premier Betting , James Mbalwe Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Board of Tanzania - GBT) na Phares Magesa, Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF).

Viwanja hivyo vitajengwa na kampuni ya Premier Betting kupitia mradi wa Premier Projects ikiwa ni sehemu ya kuridosha fadhila kwa jamii (CSR).

Kwa kuanzia kampuni hiyo ya Premier Betting itajenga uwanja wa kikapu Dar es Salaam itafuatia mikoa mengine yote nchini itafikiwa kwa awamu, utekelezaji wa mradi huu inatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa.

Rais wa TBF ameishukuru kampuni ya Premier Betting kwa kukubali ombi la TBF kusaidia ujenzi wa viwanja nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa moja ya melengo muhimu ya mpango kazi wa TBF katika kuinua mchezo wa kikapu nchini.

Ndg. Magesa amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa GBT kwa kusimamia na kuhakikisha Premier Betting inafikia makubaliano na TBF na amewataka kutekeleza mradi huu haraka.

Ndg. Magesa alisema tayari wameshawasiliana na Mamlaka husika za Jiji la Dar es Salaam ili kupatiwa eneo ambako uwanja huo unatarajiwa kujengwa na pia ameziomba Halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya viwanja vya michezo ili kila mkoa utakapofikiwa basi eneo la kujenga liwe tayari.

Pichani juu ni Ndg. Sami Matar Mkurugenzi wa kampuni ya Premier Betting (kulia) , Ndg. James Mbalwe Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Board of Tanzania - GBT) katikati na Ndg. Phares Magesa, Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF).

Lee Kocha Mkuu BAK @
 
Wale wa kikapuuu kazi kwenu

Asante kwa updates
 
Wale wa kikapuuu kazi kwenu

Asante kwa updates
Basketball Yenyewe Kama Imekufa Hivi, Nakumbuka Mwaka 2019, Timu ya mpira wa kikapu ya Tanzania ilifungwa mechi zote UGanda kwenye mashindano ya Kanda ya 5 afrika .

Kenya ilishika nafasi ya kwanza,ikifuatiwa na Misri, Uganda, Rwanda na mwisho Tanzania... Nawapa Taarifa Tu Wakuu
 
mzee mwinyi atufutie ile kauli ya kichwa cha mwenda wazimu
 
Kiufupi Miundo mbinu ya Mpira wa kikapo tanzania nifinyu tukianzia kwa kwa Viongozi paka vilabu ningumu kuwafikia wenzetu ulio wataja Hapo juu.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Kampuni ya Premier Betting yakubali kujenga viwanja vya Kikapu nchini Tanzania.

Makubaliano hayo yalifikiwa katika kikao kilichowasisha Ndg. Sami Matar Mkurugenzi wa kampuni ya Premier Betting , James Mbalwe Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Board of Tanzania - GBT) na Phares Magesa, Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF).

Viwanja hivyo vitajengwa na kampuni ya Premier Betting kupitia mradi wa Premier Projects ikiwa ni sehemu ya kuridosha fadhila kwa jamii (CSR).

Kwa kuanzia kampuni hiyo ya Premier Betting itajenga uwanja wa kikapu Dar es Salaam itafuatia mikoa mengine yote nchini itafikiwa kwa awamu, utekelezaji wa mradi huu inatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa.

Rais wa TBF ameishukuru kampuni ya Premier Betting kwa kukubali ombi la TBF kusaidia ujenzi wa viwanja nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa moja ya melengo muhimu ya mpango kazi wa TBF katika kuinua mchezo wa kikapu nchini.

Ndg. Magesa amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa GBT kwa kusimamia na kuhakikisha Premier Betting inafikia makubaliano na TBF na amewataka kutekeleza mradi huu haraka.

Ndg. Magesa alisema tayari wameshawasiliana na Mamlaka husika za Jiji la Dar es Salaam ili kupatiwa eneo ambako uwanja huo unatarajiwa kujengwa na pia ameziomba Halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya viwanja vya michezo ili kila mkoa utakapofikiwa basi eneo la kujenga liwe tayari.

Pichani juu ni Ndg. Sami Matar Mkurugenzi wa kampuni ya Premier Betting (kulia) , Ndg. James Mbalwe Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Board of Tanzania - GBT) katikati na Ndg. Phares Magesa, Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF).

Lee Kocha Mkuu BAK @
Waje kujenga na huku chato
 
Back
Top Bottom