Kampuni ya Meta kupunguza wafanyakazi na kuanza mbadala wa Akili Mnemba AI

Wild Flower

JF-Expert Member
Jul 20, 2023
372
751
Meta imeanza kufuta maelfu ya nafasi za kazi huku kampuni hiyo kubwa ya mitandao ya kijamii ikichukua msimamo mkali dhidi ya wafanyakazi wanaoshindwa kufanya vizuri na kujiandaa kifedha kwa ajili ya uwekezaji mkubwa zaidi katika teknolojia ya AI mwaka mwingine. Wafanyakazi waliathiriwa barani Ulaya, Asia, na Marekani wameshaanza kuarifiwa.

Mark Zuckerberg anawalenga wafanyakazi wenye utendaji duni, ikiwa ni sehemu ya mwelekeo mpana wa sekta kuelekea kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Kampuni imeeleza kuwa itapunguza karibu 5% ya wafanyakazi wake, ambayo inaweza kumaanisha kwamba takriban wafanyakazi 4,000 watapoteza kazi zao.

=================For English Audience====================

Meta lay offs have begun.

Meta has begun to cut thousands of jobs as the social media giant takes a tougher stance on underperforming employees and readies its finances for another year of heavy AI investment. Affected employees in Europe, Asia, and the US have started to be notified,

Mark Zuckerberg is targeting low performers, part of a broader industry move toward leaner operations.

The company has said it will eliminate roughly 5% of its workforce, which could mean almost 4,000 employees lose their jobs.

SOURCE: BUSINESS INSIDER
 
Binafsi nimeshaanza kujishudhukisha na ufugaji
Screenshot_20250201-220202.jpg
 
Tunapoelekea tutarudi kwenye barter trade sasa, wewe una teknolojia mimi nina shamba. Unanipa teknolojia yako mimi nakupa chakula.

Maana hawa wafanyabiashara washajiona miungu watu wakati hela ni karatasi la kuchapishwa tu.

Masikini akitaka kitu kutoka kwako akufanyie kazi, wewe ukitaka kitu kutoka kwake unachapisha karatasi unaliita hela unampa. Kama sio ujinga ni nini.
 
Back
Top Bottom