TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 7,332
- 14,254
Kampuni ya magari ya umeme ya China imetengeneza betri ambayo inawezesha gari kutembea zaidi ya Kilomita 1,000 bila kuhitaji chaji.
Umbali huu ni sawa na kutoka Dar mpaka Shinyanga bila kuchaji gari. Au ni sawa na kusafiri Dar mpaka Arusha; au kutoka Dar na kwenda Dodoma, na kurudi tena Dar bila kuchaji gari.
Kampuni ya Neo, ni kampuni ya China ambayo inashindana na Tesla, wiki hii CEO wake ambaye pia ndio muanzilishi wa kampuni hiyo Ameifanyia majaribio kwa kuendesha gari ya Neo ET7 kwa masaa 14 na kutembea Kilomita 1,044 kutoka Mji mmoja wa China kwenda katika mji mwingine bila kuichaji na ikabaki 3% ya charge akiwa amefika katika mji mwingine.
Neo pia ni kampuni ambayo inatumia betri ambazo unaweza kuitoa na kuweka battery nyingine, swapp betri iliyochajiwa, zinabadilishika bure; na inaruhusu mtu binafsi kununua aina mbalimbali za betri ambazo zina aina mbalimbali za uwezo. Tofauti na Tesla ambayo hauwezi kubadilisha betri yake. Pia ina gari ya umeme inayoongoza kwa speed.
China inaongoza katika teknolojia za betri za magari ya umeme na Neo imekuwa ni mfano mkubwa wa maendeleo yake. Neo itaanza uzalishaji wa betri hiyo ya 150kWh kuanzia April 2024.
Gharama ya betri hiyo ni dola 42,100$ ambayo ni sawa na gharama ya Tesla Model-Y nchini China.
______________