JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,696
- 6,491
Kumekuwa na kusitasita jinsi ya kushughulikia changamoto ya watoto wa mitaani ambao asilimia kubwa wamekuwa wakifanya kazi ya kuombaomba.
Nimelazimika kusema hilo baada ya kuona kuna Mdau wa JamiiForums.com akizungumzia changamoto kama hiyo Mkoani Mbeya ambapo alisema imefikia hatua baadhi ya Watoto hao wamekuwa wakijihusisha na matukio ya uhalifu.
Hapa Mwanza licha ya uwepo wa Kampeni maalum ijulikanayo kama 'Mchukue Mtoto Mrejeshe kwa Wazazi Wake' yenye lengo la kuwaondoa watoto mitaani na kurudi kwenye malezi bora, bado kumekuwa na changamoto nyingi katika utekelezaji wake.
Watoto hao wameendelea kuonekana katika maeneo mbalimbali hasa ya Nata na Mataa mapya ya Nera, Barabara ya Jomo Kenyatta na wanaonekana wakati wote na Wananchi tunajiuliza maswali mengi juu ya kampeni hiyo.
Kampeni hiyo ilikuwepi tangu wakati CPA Amos Makalla akiwa Mkuu wa Mkoa Mwanza mpaka leo sijui mwelekeo wake upoje.