Kamati ya kuchunguza mkataba wa Lugumi hadharani

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487

Kamati ya kudumu ya Bunge inayoshughulikia Hesabu za Serikali (PAC) imeunda kamati ndogo ya watu tisa itakayochunguza kwa kina mkataba uliozua utata wa Sh37bilioni ulioingiwa baina ya Jeshi la Polisi na Lugumi Enterprises.

Pande hizo mbili, Jeshi la Polisi na Lugumi Enterprises, ziliingia mkataba huo kwa ajili ya kufunga vifaa 108 vya kuhifadhia alama za vidole katika vituo vya polisi.

Akizungumza na wanahabari leo mjini Dodoma, makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Aeshi Hilary amesema kamati hiyo itafanya kazi kwa siku 30, kuanzia Jumatatu ijayo.

Wajumbe tisa wa kamati hiyo ndogo ni; Japhet Hasunga (Vwawa-CCM), wengine wa CCM ni Livingstone Lusinde (Mtera), Stanslaus Mabula (Nyamagana), Haji Mponda (Malinyi) na Hafidh Ali Tahir (Dimani).

Wabunge wa upinzani waliopo katika kamati hiyo ni Nahenjwa Kaboyoka (Same Mashariki-Chadema), Musa Mbaruk (Tanga Mjini-CUF), Tuza Malapo (Viti Maalum-Chadema) na Khadija Nassor Ali (Viti Maalum-CUF).

Source: Mwananchi
 

Tuwape nafasi wafanye kazi. Wamepewa siku 30 inabidi wazame ndani kabisa na ukweli wote uwekwe hadharani. Naona kuna wajumbe makini hapo kama Mh. Japhet Hasunga na Mh. Kaboyoka. Hivi ni vichwa.
 

Hivi kuna wabunge kutoka chama cha CUF wanaohudhuria vikao vya Bunge? Lilitolewa tangazo kwa umma kuwa wabunge wote kutoka chama cha CUF hawatahudhuria vikao vya Bunge la Muungano ili kuonyesha jinsi ambavyo hawakuridhishwa na mambo ya uchaguzi visiwani Zanzibar. Mbona statement ya kubatilisha haijatoka???
 
Hivi hawa wajumbe wa kamati huchaguliwa na nani ni spika au vyama hupendekeza majina ya wajumbe
Kifungu cha 117 cha Kanuni za bunge 2016 ibara ya 18 kinasema;

(18) Kamati yoyote inaweza kuunda Kamati Ndogo kwa ajili ya utekelezaji bora wa Shughuli zake, kadri itakavyoona inafaa na kila Kamati Ndogo itapangiwa kazi zake na Kamati ya Kudumu inayohusika.

Kwenye sehemu ya Majukumu ya Kamati ndogo pamoja na mambo mengine inasema;
‘’shughuli zote zinazofanywa na Kamati Ndogo zilizoundwa na Mheshimiwa Spika au Kamati husika ili kufanya kazi maalumu’’.

Kwa hiyo basi kujibu swali lako, Spika wa bunge ndiye huridhia wajumbe wa Kamati ndogo.

Ielewe pia kuwa hao wajumbe wa Kamati Ndogo ni miongoni mwa wajumbe wa PAC.
 
Hawa ni wabunge wa CUF wa kuchaguliwa na viti maalum kutoka sehemu ya Tanzania Bara na Zanzibar kwenye Bunge la Tanzania.
 
du, kamati inaunda kamati. je kunatofauti gani na enzi za jk tume kuunda tume?
 
Tuwape nafasi wafanye kazi. Wamepewa siku 30 inabidi wazame ndani kabisa na ukweli wote uwekwe hadharani. Naona kuna wajumbe makini hapo kama Mh. Japhet Hasunga na Mh. Kaboyoka. Hivi ni vichwa.
Mbina TORs alizotaja makamu mwenyekiti ni kama ni kamati ya kuthibitisha yaliyosemwa na jeshi la polisi badala ya uchunguzi?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…