Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,805
- 13,574
Ujenzi huo ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) ulianza Mei 12, 2023 na unatakiwa kukamilika Desemba 10, 2024.
"Tunawapongeza kwa kazi nzuri iliyofanyika na inaonekana lakini msisitizo wetu ni muda. Mkandarasi amalize kazi kwa muda uliopangwa" amesisitiza Mhe. Mnzava.
Naye, Waziri wa Maliasili na Utalii , Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesikitishwa na kitendo cha kuchelewa kwa mradi huo huku akimtaka mkandarasi kukamilisha kwa wakati la sivyo sheria itachukua mkondo wake.