Kamati ya Bunge: Bwawa la Nyerere litakamilika Juni 2024, Tsh. Trilioni 5.85 zimelipwa tayari

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,804
NISHATI: Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dkt. David Mathayo amesema Utekelezaji wa Mradi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP), umefikia 95.83% na utakamilika Juni 2024 huku Tsh. Trilioni 5.85 (89.24%) zikiwa zimelipwa kwa Mkandarasi.

Amesema, Kamati ya Bunge imejulishwa kuwa Ujazo wa Maji umefikia Kina cha Mita 167 kutoka usawa wa Bahari, kiasi kinachoruhusu kuanza Uzalishaji wa Umeme na Mtambo wa Kwanza utawashwa Februari 16, 2024, wa Pili utawashwa Machi 2024 ambapo Megawati 470 zitaingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

Kuhusu hali ya Umeme hadi kufikia Desemba 2024, uwezo wa Mitambo ya Kufua Umeme kutoka Vyanzo mbalimbali ulikuwa Megawati 1,889.84 ikiwa ni ongezeko la Megawati 195.29 kutoka Megawati 1,694.55 zilizokuwepo mwaka 2022.

Hata hivyo, Uzalishaji wa Umeme nchini bado ulikuwa chini ya Wastani wa Megawati 1,200 wakati Mahitaji ya Umeme ni Wastani wa Megawati 1,482.80, hali inayosababisha upungufu wa Nishati hiyo nchini kote kwa Megawati 283.

PIA SOMA

TUHUMA ZA UFISADI NA HUJUMA

HISTORIA

Aibu sana inaonyesha jinsi gani sio wastaarabu then viongozi wanategemea watendaji wawe wakweli na waadilifu kwa style hizi za kudanganyana danganyana. Si uungwana kabisa.
 
Kila siku ahadi, hii serikali inatuona wananchi Kama vimada vile
 
Kutokana na ripoti ya Mhe. Mpina Mkandaarasi alikuwa anadaiwa mabilioni kadhaa kwa kuchelewesha utekelezaji wa mradi. Je fedha anazodaiwa ni shillingi ngapi na je atawajibika kukatwa pindi atakapokamilisha/kukabidhi mradi?.
 
Nje ya mada, huyu David Mathayo si ndiyo majuzi kule Same wananchi wake wamemwambia Makonda hawamtaki??
 
Back
Top Bottom