GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,216
Katika Mtu ambaye GENTAMYCINE nimepanga nisiwe namsema ( namsiliba ) hapa JamiiForums kutokana na kuwa ni Mdau wangu mkubwa wa Miziki ya Congo DR ( Misebene ), Mwana Simba SC Mwenzangu na Mtoto wa Mjin vile vile ni Wewe Amos Makalla ( Mkuu wa Mkoa mpya wa Dar es Salaam )
Pacha ( Mdau ) Amos Makalla nimesikitika sana na Taarifa niliyoiona katika Mitandao mbalimbali ( japo bado naithibitisha ) kuwa umesema kuwa kila baada ya Miezi Mitatu utakuwa unakutana na Wazee wa CCM ili uchote Uzoefu wao na Wakufunde zaidi.
Tafadhali sana Pacha ( Mdau ) Amos Makalla kwa hili utaharibu na Mimi GENTAMYCINE kwa Heshima na Taadhima nakuomba libadilishe na badala yake kutana tu na Wazee wote bila kuweka Itikadi ya Siasa uliyonayo hasa ukiwa ni mwana CCM Mwenzangu.
Pacha ( Mdau ) Amos Makalla Wewe ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na siyo Mkuu wa Mkoa wa CCM Dar es Salaam na nimeshtuka mno kuona Mtu kama Wewe umekuja na wazo la ' Kiubaguzi ' na la ' Kipuuzi ' pia kama hili ambalo binafsi pia bila Urafiki wala Kukuonea Aibu niseme tu kuwa limenikwaza zaidi.
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere huko nyuma alipenda sana Kukutana na Wazee mbalimbali na hakuwahi ' Kuwabagua ' kwa namna yoyote ile hali ambayo iliwautia Wazee wengi bila kujali tofauti zao za Kiitikadi, Kiukabila na Kidini Kujumuika nae na kumpa Mawazo ( Ushauri ) ambao ndiyo ulikuwa Chachu ya kumfanya atuongoze vyema kama Taifa na Watanzania mpaka leo hii tunamkumbuka na hata wakati mwingine Kumlilia.
Pacha ( Mdau ) Amos Makalla nani alikuambia kuwa Wazee wa Vyama vya Upinzani waliopo hapa Mkoani Dar es Salaam hawana Mawazo mazuri ya Kukushauri tena huenda hata ya Kuwazidi hao Wazee wa CCM ambao Wewe unawaona ni bora Kwako kwa Sisi tunawajua kuwa wengi wao ni Wanafiki watupu na wakija Kukutana nawe sana sana watakachokuwa Wanakushauri ni Umbea, Majungu, Uzandiki na kukuonyesha aina mpya ya Waganga wa Kienyeji ili uende ' Ukajigange ' zaidi kusudi ' Mama ' asiwaze kabisa ama Kukuhamisha na Kukutumbua.
Usianze vibaya mapema yote hii Pacha.