Kamanda Sirro; Huu mnada wa vifaa vya magari mtaa wa Mafia na Msimbazi piga marufuku unaongeza wizi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
56,821
30,804
Kwako kamanda incharge sirro

Shikamoo baba wengine husema hozza....

Baba leo nimeona nikupe hii michongo ya wezi wa magari na vifaa vya magari

Kama mlinzi wetu mkuu nakuomba nikujuze kuna mnada unaoendelea kila siku pale Msimbazi na mafia na hata wamekuwa na sehemu inaitwa mnadani pembeni ya Bigborn.

Hawa jamaa huiba usiku majumbani mwa watu na kuuza hivi vifaa hapo.Inasikitisha kamanda mstaafu alikuwa na taarifa mezani sidhani kama amekupa kwenye handover sababu akuna kilichofanyika.

Hawa watu hawana tofauti na wezi wa bandarini wanaoiba vifaa vya magari yetu. Kamanda Sirro huu mnada kuna watu wakubwa wanahusika sipendi kusema zaidi ila hata kituo chako kikuu pale Msimbazi wana taarifa za hii sehemu na kesi zake.

Nikujuze tu 2013. Walimuibia kaka yangu kioo Kimara Mwisho.Nilipowahi tukaambiwa mzigo wa Kimara mwisho haujaja. Mmoja wa wahusika akaniita pembeni..namuona kama kaka yako atapanic muweke sawa akikiona asipige kelele akuachie muelewane nao uondoke na kioo chenu.

Haikuchukua muda pickup ikaja na vioo sita, ikashusha lundo la taa na spare kadhaa.

Baadae tukapelekwa tukakuta kioo chetu, kaka hakuamini ila nashukuuru alikuwa mvumilivu. Jamaa wakataja bei yao tukalipa nusu tukachukua kioo.

Akaja mwingine akakomaa kioo changu wakamuweka sawa tuonyeshe unapotaka tupeleke ukweli aligoma na walipokaribia nje wakakiachia chini naona.

Tunaomba simamieni ondoeni huu utapeli wa miaka yoote. Kama kuna mkubwa nani anasimamia haya?
 
Nafikiri ni vyema kama utalifikisha moja kwa moja mezani kwake. Ujasiri wako utasaidia Watanzania Million 5 wa DSM
 
Hao wezi mnawalea sana mimi navunja miguu yote yani mpka magazine iishe......maisha yake yote atamalizia kitandani kwake
 
Huu mchezo ni rasmi na naunagana namto hoja kabisaa.
Tena umeenea sehem kubw asana.
Nakumbuka niliwahi kusafirisha Carry basi walilamba mpaka mfuniko wa radiator naitoa Dar bandarini nakuta olaa.
Jamaa akaniambia utakuta mjini madukani mzigo wako unauzwa.
Hawa watu wanakera sana aisee,na huu ni mradi rasmi wa wizi na unatambulika.Maana muuzaji haya ukimuambia unauzwa kwa mnada mali umeitoa wapi?hana jibu maana kama ni Used from Dubai basi lazima aonyeshe lini mzigo umeingia na stakabadhi,ila pale uhuni mtupuuu
 
Hozza maana yake nini mkuu?
 
HII THREAD MOD SI.MLIIFUNGA NANKUNIPIGA BAN

LEO MMEONAA INA UMUHIMU..HATA NIKITAKA KUIFUNGUA INASEMA SINA PERMISSION

KUNA MMOJA WENU KALAMBWA NN ..NILISEMA MWANZON NIKITUKANA HUMU MNIONDOE MILELE ILA KAMA SIJATUKANA BASI ACHANEN NA VIBAN VYA SIKUTATU NNE MNAFUNGA NA THREAD LEO MNAIACHIA

HII N WEAKENESS KAMA SHIDA ILIKUWA JINA LA KAMANDA HUYU N BOSIWETU WOTE WANA DAR ES SALAAM
 
Hili jeshi la polisi lilitakiwa lifanyiwe reshuffle kama alivyozungumza kamanda fulani mstaafu wa jeshi hilo maana kuna maeneo hayako sawa.
 
Wizi huu ni majanga. Kuna jamaa tabata kasema ya raum yake ameikuta juu ya mawe na siti zote wameng'oa
 
Kuna siku nilikuja dar,maeneo ya flani familia yangu mwanzo ilipokua,,bahati mbaya nikapishana na wife kitu flan na ukweli nilichukia sana,ikabidi usiku huo huo nitoke niende kwa msela wangu kulala kule,,lkn ile nawasha gari wazo likanijia kua nikienda kulala kule ntazua mengi zaid,,nikarudi ndani nikachukua funguo ya gari yake sababu seat zipo nying ndani (ipsum new model) nikalala seat zile za nyuma kabisa,,mida ya saa 9 usiku nasikia kama kitu kinakorokocha iv,nikastuka naona kama tochi zinawaka waka ndani ya gari,kucheki vizur nje nako wanakomaa kutoa mabamper na taa,,nikachukua simu yangu nikapunguza mwanga mpaka mwisho,

Nilikua nimevaa sweta lain,nikalivuta mpaka uson nikaweka silent simu alafu nikatuma text kwa jilan zangu kadhaa alfu nikaanza kupiga simu zao ili waone text,wakipokea nakata,,mmoja akajibu poa ngoja atafute kikosi,,walipokaribia wakatuma text tupo nje,,mmoja yumo ndani anakomaa na dashboard na hajaniona,nikawapa direction wakazama uwan,tuliwakamata kama kuku,tulitoa kipigo heavy,mmoja alikufa na wale watatu police waliai kuwaokoa,,lkn kuna afande mmoja alisema hawa washatusumbua sana,,muwe mnatuita mkishamaliza kila kitu,,walikua na hilux yao nayo tukapiga kiberit yote ikateketea,watu walikua na hasira sana..
 
wanakuwa wa foo sana sometimes
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…