Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, amesisitiza kuwa kifo cha mfanyabiashara Daisle Ulomi aliyetoweka katika mazingira yenye utata Desemba 11, 2024 akiwa kazini kwake Sinza Kijiweni, kimesababishwa na ajali na si vinginevyo.
“Ukiniambia simu ilisoma wao ni watu wa TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania), hao ndugu unaodai simu ilisoma Chang’ombe ni watu wa TCRA? Sisi ndiyo tunasema ajali ilitokea hapo Ubungo External Makuburi. Kuna kundi la watu wenye tabia ya uzushi lenye nia ya kuzusha kwa malengo ya kuzua taharuki.
Soma Pia:
- Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala
-
Familia ya Ulomi yakubali ndugu yao amefariki kwa ajali
Tukio limetokea mchana kweupe wasamaria wema wamejitolea wenye ubinadamu, wenye utu, licha ya kwamba ilikuwa ni ajali mbaya,” amesema SACP Muliro.
Kamanda Muliro amezungumza hayo leo Jumanne Desemba 17, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa watu wasitumie hisia na kwamba hakuna ubishi Ulomi amekufa kwa ajali.