NIKIWA MMOJA WA WATANZANIA WALIOPOTEZA WAPENDWA WAO KWA AJALI ZA BARABARANI HUSUSAN ZINAZOHUSU MABASI YA ABIRIA, NAJIKUTA SINA JINSI ILA KUTAKA KAMANDA WA USALAMA BARABARANI KITAIFA MOHAMED MPINGA AWAJIBISHWE AMA AJIUZURU MWENYEWE KWA KUSHINDWA KAZI.
KATIKA HISTORIA YA NCHI HII HAKUNA KAMANDA WA TRAFIII ALIYEKUMBWA NA MIKASA MINGI YA AJALI KAMA HUYU AFANDE.
IWEJE KILA KUKICHA NI AJALI TU LAKINI HAKUNA HATUA STAHIKI ZA MAANA ZINAZOONEKANA KUCHUKULIWA.
KILA NJIA NCHI NZIMA KUMEJAA VITOCHI VICHAKANI NA MABILIONI YA FAINI YANAKUSANYWA, LAKINI KWA VILE UKILIPA ELFU 30 YAO UNAPETA HAKUNA ANAYEJALI NA AKIONDOKA TU ANAKANYAGA MOTO.
KAMANDA MPUNGA AKIONDOKA ATAEMRITHI AFUATE MBINU ZA MWENDOKASI DAR AMBAKO AJALI SASA NI NADRA MNO NA KUTUMIA NJIA YA MABASI HAKUNA TENA! KISA? MWENDO KASI NI JELA BILA FAINI. NA HIO NDIO DAWA