Kama unawapenda watoto wako usiwalete Duniani!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,785
Huw najiuliza. Kama maisha ya Duniani yamejaa kila aina ya taabu na mahangaiko! Njaa, vita, magonjwa n.k kwa nini bado binadamu wanapendelea kuzaa tena wengine wanapenda kuzaa watoto wengi?
Mimi nikaona njia njema ya kuwalinda watoto wetu tunaowapenda kwa mioyo yote ni kuwaacha huko huko walipo bila ya kuwaleta Duniani.
Maana hata baada ya kutoka hapa Duniani kuna adhabu ya ahera inawasubiri iwapo hawatofanikiwa kuingia peponi...
Dada zangu embu tushirikiane kwa hili... Duniani hakuna cha muno kiasi cha kuleta watu ambao 'hawana chao' humu...
 
Unazungumzia watoto gani hao?

Halafu, umeshawahi kuwashirikisha wazazi wako hili wazo?
 
Unazungumzia watoto gani hao?

Halafu, umeshawahi kuwashirikisha wazazi wako hili wazo?
Watoto walioko kwenye viuno vyako na kwenye ovary kwa upande wa mwanamke...
Wee! Wazazi wanavyopenda wajukuu unaanzia wapi kwa mfano?
 
Watoto walioko kwenye viuno vyako na kwenye ovary kwa upande wa mwanamke...
Wee! Wazazi wanavyopenda wajukuu unaanzia wapi kwa mfano?
Hizo cell unazozingumzia sio watoto mkuu..!
Mtoto anapatikana pale hizo cell zinapoungana..!

Hata hivyo tukienda mbali zaidi, hata hizo cell ili ziwepo lazima kuwe na mtoto alizaliwa miaka mingi iliyopita...!
La sio hivyo hata wewe sidhani kama ungekuwa hapa unachat na mimi.
 
Mkuu una miaka Mingapi.......naona tu km bado una mawazo ya kitoto kidogo...
Coz kwa hayo mawazo huwezi mshauri msichana/mwanamke azeeke bila mtoto au MTU tajiri azeeke bila mwanae,Sasa Urithi wake atamuachia Nani...?
 
Its simply called faith in God.

Na sio katika kuzaa tu. Katika mambo mengi ambayo ni Mungu tu huwa anayaendesha na kuyaweka sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…