Kama ulizaliwa baada ya 1995 mambo haya yalikupita

Ceas

Senior Member
May 5, 2019
193
205
Wale mliozaliwa miaka ya 1995 kurudi nyuma mnayakumbuka haya?
1. Kung'oa jino kwa kutumia Uzi
2. Kupamba kadi na pamba sebuleni
3. Ubwabwa kupikwa jumapili tu
4. Ukumbi wa starehe kupambwa kwa toilet paper
5. Kunyolewa kwa mkasi
6. Kufunga hela kwenye leso au pindo la kanga
7. Wavulana kuvaa nguo ya ndani ya aina moja (VIP) usiombe ikakatika utakuta imebana kifua
8.Kurewind kanda kwa peni
9. Nchi nzima kuangalia movie ya komando John, double impact, Rambo na Blue three.....
10. Watoto wote wa mtaa mmoja kufahamiana kwa sababu ya kucheza kombolela na kibaba baba...
11. Kukata ndala kuwa mfutio
12. Kunyolewa msalaba ukiwa na nywele ndefu
13.Shati la shule kuweka vibox mgongoni
14. Kuchomolea shati nyuma
15. Kuweka shati la shule blue
16. Kusimamisha kola ndio ubitozi/usela
17. Ukimuandikia barua kwa umpendaye lazima uchore moyo na mkuki na lazima upulizie pafyumu ya "Yu"
18. Hata kama mligombana January unaambiwa subiri shule ifunge.

Je wewe unakumbuka kipi?
 
Nacho kumbuka ratiba za video za mikanda ya ngumi, na boringo za kina pepe kale zililuwa zinaonesha kwa awamu.

Leo kata hii, kesho kata ile, kesho kutwa yake kata ile tena nyingine



hahahahaa hii kali...hii ndo naiskia kwako hahahaha...mienakumbuka shule weknd matron anawawekea mikanda ya mafundisho..mfano ya ukimwi..au mkanda wa Yesu..hahhaha...mkanda wa Yesu had ĺ eo nikiuskia sehem neno linalofuata nalijua ..yaa niliushika balaa...doh .
 
nimekosa vingi:oops::oops:
ila hiyo 14 nilikua nachomolea kwa mbele
shuleni kwetu hakuna kupigwa mkasi ni unanyang'anywa begi mpaka ukanyoe na saloon ipo ndani ya shule,,kama huna ela utakopa tu
 
Back
Top Bottom