Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,340
- 118,614
Wanabodi,
Tanzania ni nchi inayofuata Katiba na kuendeshwa kwa utawala wa sheria, hivyo itaongozwa kwa mujibu wa Katiba, sheria taratibu na kanuni!, no one is above the law!. Katika kufuata sheria hizo, taratibu na kanuni, pia kuna mamlaka ambayo katiba imempa rais wetu wa JMT kuyatekeleza at his pleasure, yaani vile rais atakavyoona inafaa, ikiwemo presidential appointments powers, and the power to hire and fire civil and public servants!.
Hata kama Dr. Magufuli ni rais wetu, haina maana ana inherent powers kuamua chochote na watendaji walio chini yake kazi yao ni kusema tuu "'YES!", "ndiyo mzee!". Wasaidizi wa rais, wanawajibu wa kumsaidia rais kutimiza majukumu yake ya urais kwa mujibu wa katiba kama alivyoapa kuilinda na sio kufanya kama anavyojisikia yeye!.
Kwa hali ninayoiona sasa, Rais Magufuli anakoelekea, asipodhibitiwa, na vyombo vya udhibiti ambavyo ni Mhimili wa Bunge na Mhimili wa Mahakama, very soon kuna watu sio tuu watalia na kusaga meno, bali Tanzania kama nchi na taifa, tutaumia!.
Jee kuna ubaya tukimshauri rais wetu, kama huu anaoufanya sio udikiteta?!, then ni bora sana, Mhe. Rais aka "Futilia Mbali Utawala wa Sheria, akaiweka katiba pembeni kwa muda kidogo tuu (wa miaka 20 au 30, sio kama Mugabe, Kageme au Museveni,)kwa kutangaza hali ya hatari?!", na ndipo sasa ainyooshe nchi, na ikiisha nyooka ndipo airejeshe katiba.
Katiba imempa mamlaka kutangaza hali ya hatari hivyo katiba huwekwa pembeni na badala yake nchi huongozwa kwa kutumia Presidential Decrees!, yaani amri za rais, ambapo kila anachokitaka rais na kukisema kinaandikwa na kinakuwa sheria!, kiukweli akilifanya hili, atafanikiwa sana kuinyoosha nchi hii ambayo kiukweli ilikuwa imepinda sana!.
Rais alipoamuru zile pesa "private money", zilizochangwa na private entities, zikiwemo public corporations, kama sehemu ya CSR zao kuwakirimu wabunge wapya kwa mlo wa usiku!, alitumia sheria gani na mamlaka gani?!. Yaani rais anaweza kuamuru private money toka private entities watumieje fedha zao?!, kwa mamlaka ipi!?, kupitia sheria ipi, kanuni ipi na taratibu zipi?!. Huu kama sio udikiteta ni nini?!. Rais anafanya udikiteta anashangiliwa?!, ni Tanzania pekee!.
Rais alipoamua hayo, wengi wameishia tuu kusifu, kushangilia na kupiga makofi, hakuna aliyejiuliza, au kuhoji, rais ametoa agizo hilo kwa mamlaka gani?!, alafu hapa tukisema Magufuli ni dikiteta tutakuwa tumemuonea?!.
Nijuavyo mimi japo rais ni rais wa nchi, na ndiye mamlaka kuu kupitayo zote katika yale yaliyo ya Kaizari, ila hiyo mamlaka sio kwenye kila kitu bali kwa kupitia chaneli rasmi, mfano serikali ina mihimili mitatu ya Serikali, Bunge na Mahakama, sasa ni kwenye serikali kuu na serikali za mitaa pekee, ndiko rais ana mamlaka kuu ya "inherent powers", ambayo ni mamlaka kamili yanayoitwa "eyes on and hands on", anaweza kufanya lolote bila kuulizwa na yeyote!. Serikali ni yake anaweza kuifanya vyovyote apendavyo ikiwepo ku hire and fire vyovyote anavyojisikia.
Kwa mihimili wa Bunge na Mahakama, rais pia ana mamlaka ya "eyes on na hands on", only through wakuu wa mihimili hiyo, mahakama kupitia uteuzi wa Jaji Mkuu, na Bunge kupitia uteuzi wa Katibu wa Bunge, Rais hana mamlaka yoyote kumwingilia Spika wa Bunge, hii inamaanisha rais hawezi kuamua jambo linalolihusu Bunge bila kupitia kwa Spika, au Jambo linaloihusu mahakama bila kupitia kwa Jaji Mkuu, mfano lile katazo la kuwakataza watumishi wa umma kusafiri nje bila kibali cha chake kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, lilipaswa kuuhusu mhimili wa serikali tuu, mhimili wa Bunge walipaswa waombe kibali kwa Spika kupitia kwa Katibu wa Bunge na mhimili wa Mahakama uombe kibali kwa Jaji Mkuu kupitia kwa Msajili wa Mahakama!. Kitendo cha Spika na Jaji Mkuu kutakiwa kumpigia magoti Katibu Mkuu Kiongozi, sio tuu ni dharau kwa viongozi hao, bali ni udikiteta wa mkuu wa mhimili mmoja kuingilia utendaji wa mihimili mingine!, kitendo cha udikiteta kunyamaziwa na vyombo vyenye jukumu la kum check rais, if no one can check him, kuna siku ataingilia mamlaka za zile taasisi independent kwa mujibu wa katiba yetu ikiwemo ofisi ya AG, DPP, CAG, Takukuru, Ethics Secretariat etc na hakutakuwa na yoyote atakayethubutu kukohoa, matokeo ya mwisho ya udikiteta wa aina hii ni rais Magufuli kubadilika toka a benevolent dictator alivyo sasa into a real dictator, atakuwa Bunge ni yeye na atakuwa Mahakama ni yeye! ,only God knows!.
Tunapokuja kwenye mashirika ya umma na makampuni , hizi japo zinamilikiwa na serikali, ni private bodies, zenye mamlaka zake zinazojitegemea kupitia bodi zake, hivyo mamlaka ya rais ni "eyes on, hands off", serikali inaweza kuchungulia tuu kile kinachoendelea ndani ya taasisi hizo, kwa rais kuwateua wakuu wa taasisi hizi na wenyeviti wa bodi, na sio kutia mkono ndani ya uendeshaji wa taasisi hizo. Na ikibidi rais kutia mkono ndani ya taasisi hizo kuzuia madudu, then rais anaingiza mkono kupitia kwa waziri wa wizara husika, kuilekeza bodi husika iieleza menejimenti ya shirika husika au kampuni husika!, au rais kumfire Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi wa taasisi hiyo lakini sio kuingilia mambo yake ya ndani.
Mashirika haya yanatenga fungu fulani za kufanya shughuli zao za CSR ili ku achieve specific objectives kwenye strategic plans zao!. Kama Bunge ambalo ni taasisi huru na mhimili unaojitegemea, liliomba udhamini wa sherehe ya mlo wa usiku toka kwenye mashirika na makampuni, kisha mashiika na makampuni hayo wakaona ombi la Bunge lina fit kwenye zile CSR zao, wakatoa fedha zile, rais anakuwa hana mamlaka kabisa ya kuingilia Bunge na kuamuru different use ya private money?!. Rais alichofanya ni udikiteta tuu na ubabe tuu.
Hata kama rais ameona matumizi yale yalikuwa ni anasa tuu, hana mamlaka ya kuliingilia Bunge, bali ana uwezo wa kumuita Spika na kumuomba Bunge lisifanye matumizi mabaya ya fedha, na Spika akubali, rais hawezi kumuamuru kitu Spika wala Jaji Mkuu, hivyo Spika ana hiyari akubali au akatae ombi la rais. Akikubali then Bunge liziandikie tena zile taasisi kuziarifu kubadili matumizi ya zile fedha za michango hiyo, na hakuna taasisi ingekataa kwa sababu ni jambo jema. Na kama kuna taasisi ingegomea ingerudishiwa fedha zake ili zipangiwe CSR nyingine, na rais kama rais hata kama alihitaji hizo fedha zipelekwe kuhudumia wagonjwa Muhimbili wenye uhitaji mkubwa zaidi wa vitanda kuliko mlo wa wabunge, rais hana mamlaka hayo aliojipa kuliingilia Bunge, rais naye angeweza kuomba fedha toka mashirika au taasisi hizo kama wanavyofanyaga kuomba fedha kuifadhili CCM nyakati za uchaguzi!, lakini sio kuliingilia Bunge na kuamuru hayo matumizi mengine kwa fedha hizo, au Bunge baada ya kuipokea michango hiyo, Bunge ndilo lingeamua badala ya kufanyia sherehe, wakanunulie vitanda vya wagonjwa lakini sio rais kutoa amri kuliingilia Bunge, huko ni kuingilia mamlaka ya mihimili mingine!, huu ni udikiteta!.
Baada ya kufanikiwa kwenye hili na kupongezwa, leo rais wetu ameibuka na jingine kubwa zaidi, hili ni kufuta paredi ya uhuru!. Hii iko kwenye mamlaka yake, kiukweli mwanzoni sikujua kuwa kumbe paredi ya uhuru ni miongoni mwa sherehe zinazoadhimishwa at the pleasure of the president?!. Nilifikiri hii ndio the no 1 state event ambayo ni statutory na ipo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni?!, hivi ni kweli rais wa nchi anaweza tuu kuamka asubuhi na kuamuru maandimisho ya paredi ya uhuru yafutwe kwa kauli ya mdomo just like that?!, na watu wemenyamaza?!. Japo rais anayo mamlaka kuifuta public holiday yoyote na kuigeuza ni siku ya kazi, au kuitangaza siku yoyote kuwa ni siku ya mapumziko, tangazo hilo hutolewa kwa presidential decree, taarifa ya rais kuifuta paredi ya uhuru, haina decree yoyote!. Hata kama rais anayo mamlaka hayo kikatiba, hawezi kuamka tuu asubuhi na kutoa tamko, bila decree!, sasa kitakachofuatia tamko hili, ndipo decree itatayarishwa na kuwa backdated, kisha Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu itatuleta hiyo decree siku nyingine!. Hili likitokea, nauita ni uhuni!.(uhuni huu ulifanyika)
Mnaonaje mkiungana na mimi, tumshauri rais wetu ili kuyanyoosha mambo yake vizuri, awe na mamlaka ya kufanya kila anachotaka, mnaonaje kama tutamshauri asitishe utawala wa sheria kwa muda, badala yake aongoze kwa kutumia presidential decrees pekee?!, mambo yakiisha tengamaa, ndipo turudishe utawala wa sheria?!.
Najua kuna watu humu wanaweza kulitafsii bandiko langu hili na chuki binafsi!, nawaomba sana wanisome hapa!, mimi ni mmoja wa waliosema kuwa Mgombea wa CCM atakuwa ni John Pombe Magufuli tena kwa sababu maalum. Angalia kwa makini bandiko hili ni la lini
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 ni John Pombe Magufuli-Aug 15, 2014
Na baada ya CCM kumpitisha rasmi Magufuli, nilipandisha bandiko hili
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Yaishe!.
Na baada ya ushindi wa Magufuli, nilipandisha uzi huu
Ushauri Wa Bure kwa ENL, Chadema na UKAWA, Tukubali Kushindwa, Tuyakubali Matokeo...
If You Can't Beat Them, Join Them!, He is a Worst Dictator!.
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply "A Man of The People!".
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, ni vitendo Bila Kuchelewa!.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kweli Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli atimize majukumu yake kwa mujibu wa katiba.
Paskali