Kama rais anaweza kufuta hifadhi na kuifanya kuwa makazi, basi anaweza kuyafuta makazi na kuyafanya kuwa hifadhi.

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
23,675
55,840
Mwaka jana serikali iliifuta hifadhi ya Kigosi na kufanya kuwa makazi ya watu. Hakukuwa na kelele, badala yake watu wa makundi yote walishangilia.


Sasa rais kupitia kwa waziri wa TAMISEMI amefuta kata kadhaa na baadhi ya vijiji na kuvifanya hifadhi . Ktk maamuzi haya wilaya ya Ngorongoro imefutwa yote ( kata zake zote 11 zimefutwa).

Kama rais ndiye amekasimiwa umiliki wa ardhi yote ya Tanzania na anaweza kubadilisha matumizi yake, nini kinatushangaza kuifuta Ngorongoro? Kwann tusibadili sheria za ardhi??

Ushauri wa kuifuta wilaya ya Ngorongoro ulitolewa na CDF mstaafu Mabeyo.


 
Yas katiba inasema hivyo. Ardhi yote ni ya Rais ndiye serikali. Imekaa kifalme.

Nchi yetu sio kama Marekani ambapo watu wanamiliki ardhi yao. Huo ndio uhuru wenyewe sasa.

Tukija kubadili katiba hili nalo tulitazame. Lazima katiba iruhusu watu kumiliki mali zao kama watu huru. Na ardhi ni mali ya kwanza kabisa
 
2008 shule ya msingi manyara ranch iliondolewa katikati ya mbuga ya manyara ikahamishiwa makuyuni Ili kupisha wanyama waendelee kuongezeka na kuepusha wanafunzi kukutana na wanyama wakali..

Cjajua baada ya shule kuondolewa n nn kiliendelea pale japo nayo ilikuwa imechakaa Sanaa ujui dirisha lipi Wala mlango upi ,mabweni sasaaa
 
Back
Top Bottom