Konny Joseph
Senior Member
- Aug 28, 2016
- 118
- 197
Akichangia mapendekezo ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Mbunge wa #Gairo (CCM), Ahmed Shabiby ameishauri Serikali kukata Tsh. 2,000 kila Mwezi kwenye laini za simu na Tsh. 10,000 kukatwa kwa Wabunge, Wafanyabiashara na Wafanyakazi ili fedha hizo ziwe chanzo cha mapato ya Bima ya Afya kwa wote
Shabiby amesema kuna Wamiliki wa Laini za Simu Milioni 72 Nchini ambao makato yao kwa Mwaka yataingiza Tsh. Trilioni 1.72 na zikijumlishwa za Tsh. 10,000 kwa Mwezi za Wabunge, Wafanyabiashara na Wafanyakazi, Serikali itapata kwa Mwaka takriban Tsh. Trilioni 2.
Ni kama mzaha hoja za ajabu ajabu kama hivi huwa zinageuka kuwa sheria,bila wananchi kutarajia.
Tunakumbuka Mama Salma Kikwete alivyoibua hoja ya kuwalipa wenza wa viongozi wastaafu bungeni,na kama masihara bunge likainuka na hoja hiyo na kuifanya kuwa sheria.Leo hii mabilioni ya kodi za watanzania zinatumika kuwalipa watu ambao hawakuwa na majukumu yeyote ya kiseriakli mpaka kufa kwao.
Ni kwa namna kama hii ndio Mbunge wa Ilala,Mh.Mussa Azan Zungu alivyoleta hoja ya tozo ya miamala ya simu bungeni.Watu waliona ni masihara.Ghafla sheria ikatungwa na watanzania wanaendelea kuumia kila uchao.
Hivyo nina imani kwamba hata hili la mbunge Shabibi ambalo watu wanaona kama ni sanaa tu mda sio mrefu litatungiwa sheria na litapitishwa na bunge ili kuongeza majaraha kwa wananchi.
Jambo ambalo wanapaswa watanzania wafahamu ni kwamba hakuna mbunge wa CCM anaeibuka na hoja bungeni bila kuagizwa na serikali ya CCM.Huwa ni mpango ambao huwa umeshapangwa,hivyo muhusika hutolewa kafara ili kutekeleza maagizo.
Na hii ndio maana miswaada mingi ya hovyo ndio unaona bunge linakimbilia kuitungia sheria.Na kwa bahati mbaya nchi hii imekuwa na mahakama ya hovyo kiasi kwamba Bunge au Serikali huwa ndio mwamuzi wa mwisho wa jambo lolote linalohusu mustakbali wa nchi hii.
Hivyo watanzania wawe tayari kupokea sheria mpya ya tozo za laini za simu ili kuichangia NHIF.