Kama Muhimbili na Bandarini Kulikuwa na Changa la Macho, Zile Trilion 1.4 TRA jee ni Kweli?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,374
72,891
Mkuu wetu alitembelea Muhimbili mara tu alipoapishwa na kuona kuambiwa kuna upungufu wa vitanda 200 naye alipoenda kukutana na Wabunge akafyeka fedha zilizochangwa na taasisi mbalimbali kwa sherehe ya bunge na kwa mbwembwe vikanunuliwa vitanda 270 na tukaambiwa kuwa sasa Muhimbili kulala chini ni historia.
Kukaja hekaheka bandarini kuhusu kontena za mizigo, mwanzo kwa mbwembwe vile vile tukaambiwa na mkulu ni mia tatu na kitu zimegunduliwa kuwa zimepotea na watu tuashika vichwa kwa hudhuni kuwa 380? Zote hizo? Lakini baada ya siku chache kumbe ni zaidi ya elfu kumi na moja hazijulikani zimepitaje. Na leo tena huko bandarini mafuta nayo kumbe hata mita hazifanyi kazi kwa awamu ya pili yote ya Kikwete na limejulikana hilo siku 100 za JPM.
Sasa nauliza jee kwa usanii huu hata hayo makusanyo ya TRA ya january tunayoambiwa ni Shilingi Trilioni 1.4 kweli kuna uhakika huo au nalo ni changa la macho? Maana kama kweli serikali imekusanya kiwango kikubwa zaidi ya makisio yake sii hata ingeonekana ina fedha na kuweza kulipa madeni yake yote ya wakandarasi, waalimu na hata wakulima walio kopwa?
Au ni cooked figure ili kumrizisha mzee tuu na hakuna kitu? Hili lichunguzwe, maana mficha nanihii huwa hazai.
 
Inawezekana kweli haijakusanywa 1.4 Trillioni kwa mwezi, lakini hata kama 1.4 trilioni itakusanywa kwa mwezi haiwezi ikatumika yote mara moja.
 
Ngoja nishuke kibavichabavicha hapa, WEWE MPUMBAVU, huu uzi gani sasa?? NIMEKUTUSI TUSI kubwa sana kwa kutuaibisha binadamu!
Kama BAN wanipe tu maana siku hizi nakula sana BAN humu.
 
Ngoja nishuke kibavichabavicha hapa, WEWE MPUMBAVU, huu uzi gani sasa?? NIMEKUTUSI TUSI kubwa sana kwa kutuaibisha binadamu!
Kama BAN wanipe tu maana siku hizi nakula sana BAN humu.
Kumbe lengo lako ni kula ban na sio kuiangalia hoja? Endelea kutukana bibie!
 
Inawezekana kweli haijakusanywa 1.4 Trillioni kwa mwezi, lakini hata kama 1.4 trilioni itakusanywa kwa mwezi haiwezi ikatumika yote mara moja.
sasa kama ni hivyo kwanini mnaudanganya umma ? mmetumwa na nani na kwa faida ipi ? mnatuletea uzushi kama ule wa mabilioni ya jk , kumbe hakuna lolote ! wakati wa kampeni mlituahidi mil 50 kila kijiji , hii imefikia wapi ?
 
Ngoja nishuke kibavichabavicha hapa, WEWE MPUMBAVU, huu uzi gani sasa?? NIMEKUTUSI TUSI kubwa sana kwa kutuaibisha binadamu!
Kama BAN wanipe tu maana siku hizi nakula sana BAN humu.
kwa style hii utatandikwa BAN hadi ukome .
 
Kwa makusanyo hayo na kuweza kuzilinda zisiwnde kwenye mifuko haramu nchi inaweza kuondoka kwenye nafasi iliyopo kwa kipindi kifupi
 
Hawa ndio watu JK anamwambia Magufuli awakumbuke!!!
Na mpaka Leo hawajafanyiwa chochote na njaa haina subira. Sasa ni kutukana tuu,bado watamgeuzia kibao Mwenyekiti wao sasa kwa kushindwa kumshawishi magu
 
Na mpaka Leo hawajafanyiwa chochote na njaa haina subira. Sasa ni kutukana tuu,bado watamgeuzia kibao Mwenyekiti wao sasa kwa kushindwa kumshawishi magu
Mkuu hio trilioni inawezekana lakini ikawa ni malimbikizo yaliokwepwa ngoja wamelize madeni ndio tutajua ukweli.
 
Kamanda upo dunis gani?
Pesa za elimu bure zimetumwa
Makandarasi wameitwa site
Mahakama wamepewa hela yao na mengine mengi tu ambayo hajatangazwa
 
Kamanda upo dunis gani?
Pesa za elimu bure zimetumwa
Makandarasi wameitwa site
Mahakama wamepewa hela yao na mengine mengi tu ambayo hajatangazwa
Mkuu Niko dunia hiihii, unajua Pesa za elimu bure zilizopelekwa ni kiasi gani? Bil 18., na hizo hata makusanyo ya awali ya Bil 800-900 ilikuwa inawezekana tuu. Lakini kama alivyosema mdau hapo juu kuwa yawezekana ni malipo ya malimbikizo sawa. Ila swali linabaki pale pale jee hiyo nayo sio abrakadabra kama Muhimbili nk?
 
Mkuu tulia watu wafanye kazi utaona tu,vinginevyo itabidi uwe Tomaso
 
Mimi nilishasema mapema sana kwamba ipo siku tutatangaziwa kuwa rais ameususa urais na kuamua kurudi zake Chato...si mnamjua mzee kwa kususa. Maana uwaziri tu alishawahi kumsusia mkwere uwaziri wake
 
Mkuu tulia watu wafanye kazi utaona tu,vinginevyo itabidi uwe Tomaso
Mkuu hata JPM mwenyewe angetulia baada ya kutoa vile vitanda 200 asingekuja kugundua kumbe bado wakina mama wanalala chini na wengine uvunguni kwa aliambiwa mambo poa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…