6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,701
- 5,801
Niaje waungwana
Waungwana wenzangu, najua kuna watu wanajiuliza kwamba inawezekanaje mimi nimshauri mtu jeuri kama Benjamin Netanyahu aende akaonane na mtu kiburi kama Ayatollah Khamenei ambae ni adui yake mkuu namba 1 hapa duniani.
Obvious inaweza kuwa ngumu ukizingatia kuwa Netanyahu hataki aonekane kuwa anaenda kuomba poo kwa Khamenei, na pia huenda Khamenei asikubaliane na mpango wake wa kuonana na Netanyahu nk. Lakini ki ukweli ili Netanyahu aisitiri Israel na aweze kuishi kwa amani yeye na wazungu wenzake pale mashariki ya kati basi anahitajika sana kumuona Khamenei, iwe Iran, Saudia, Jordan au popote, wakae chini waombane msamaha, wasahau yaliopita na kukubaliana wagange yajayo kwa pamoja.
Kwanza Israel wakubali kuipatia Palestina uhuru wao, pili wahakikishe kuwa wale wayahudi wenye chuki mbaya hawavuki mipaka iliyowekwa na Umoja wa Mataifa na kwenda kuwatoa kwa nguvu wapalestina, kuwapiga, kuwakamata, na kujenga katika ardhi zao (Palestina) kinguvu kama wanavyofanya sasa hivi, hadi kupelekea Hamas kulipiza uvamizi huo kwa kuteka watu Israel na kuwapeleka kusikojulikana.
Kisha baada ya hapo wapange mipango ya kushirikiana pamoja katika maswala ya kiuchumi, kijeshi, teknolojia na kiintelejensi. Katika ushirikiano huo wa kiuchumi, kijeshi na kiintelejensi nina Imani atakaefaidika zaidi ni muisrael kwa vile muiran yuko far ahead (mbali mno) katika maswala ya kijeshi, kiuchumi kuliko muisrael. Na mifano hai ipo mingi, inaonekana kwa macho na matendo.
Mfano fikiria Iran imewekewa vikwazo vya kiuchumi kwa muda wa miaka zaidi ya 50 lakini hata siku moja hauwezi kusikia kuwa imeomba, au imepewa msaada wa fedha na US,UK wala EU. Pamoja na vikwazo, ukubwa wa nchi na wingi wa population yake lakini jamaa wanasimama wenyewe na kuhakikisha kuwa hakuna janga la njaa kama lile tunalolishuhudia hapo Ethiopia, Somalia, Kenya nk ambapo hakuna kikwazo hata kimoja.
Kwa mambo ya jeshi (ulinzi) ndio kabisa. Nchi ina vikwazo lukuki vya kuizuia kutengeneza hata sindano, lkn jamaa wameweza kutumia akili zao kutengeneza silaha ambazo hadi leo wale walioiwekea vikwazo wanaona aibu. Fikiria mtu umemzungushia mbwa nje ya nyumba yake yote ili afe na njaa, asitoke kutafuta chakula, lakini unashangaa unamkuta sokoni au dukani ananunua chakula huku wewe muweka mbwa ukishindwa kujua kuwa jamaa alipitia wapi hadi kumkuta sokoni au dukani na wakati mbwa wakali bado wameizingira nyumba yake na milango yote imefungwa. Hapo lazima utaona tu aibu badala ya hasira, maana chuki yako kwake inakuwa haijamuathiri kwa lolote 😂😂😂
Leo hii Iran hiyo hiyo ambayo ina vikwazo vya kutengeneza silaha vilivyowekwa miaka zaidi ya 50 iliyopita ndo inayo supply baadhi ya silaha kwa Urusi ili iichape vizuri Ukraine na NATO yao, hadi nchi za magharibi zinapiga kelele na kukimbilia eti kuiwekea vikwazo vingine utafikiri kuwa hivyo ndio vikwazo vya kwanza kuwekewa, kumbe hawajui kwamba jamaa kila wanavyowekewa vikwazo ndio wanavyozidi kuwaongezea akili ya kuwafanya watafute njia za kujilinda zaidi.
Iran hiyo hiyo ambayo imewekewa vikwazo vya silaha bado inatengeneza silaha kibao mpaka zingine ina supply kwa vijana wao Hezbulah, Houth Yemen, shia group Iraq, na zingine wanampa Assad bure zimlinde mpaka leo.
Hii ni tofauti na Israel ambayo haina vikwazo vyovyote vya kutengeneza, kupewa au kuagiza silaha kutoka nje. Lakini bado wamebweteka, wameshindwa kujiongeza, ili siku ikitokea kuwekewa vikwazo vya silaha hata vya mwaka mmoja, basi waweze kujitegemea wenyewe kama wenzao Iran. Toka Dunia iumbwe mpaka leo hatujawahi kusikia Israel imempa mtu au nchi msaada hata wa bomu la kurusha kwa mkono, achilia mbali ndege au kifaru. Israel imekosa silaha hata za kumpa ndugu yao (Ukraine) anaebondwa kila siku na mrusi huko Ulaya. Tunachoona ni yeye kupewa tu sio kutoa. Hii inamaana kuwa jamaa hawana watu wa maana wa kuwatengenezea silaha zao wenyewe za kujilinda. Misilaha yote tunayoona inatumika kuua kina mama na watoto huko Gaza na Lebanon zilitengenezwa Na kuletwa kutoka Ulaya na Marekani kisha wanafunza namna ya kuzitumia. Ndomaana Netanyahu anarusha rusha tu hovyo maana anapewa tu bure, hazitengenezi yeye.
Hivyo wakiwa marafiki na Iran Kisha kuomba kushirikiana katika mambo ya ulinzi, uchumi, teknolojia na intelejensia basi Israel itafaidika, na itakuwa imara maradufu kiasi kwamba hakuna nchi yoyote hapo mashariki ya kati itakayomgusa Netanyahu anaeshirikiana kijeshi na Ayatollah.
Dunia kwa sasa imeshajua kuwa ni nani mbabe wa kweli wa mashariki ya kati kupitia silaha zao wenyewe. Mfano Ayatullah aliwahi kusema mapema tu kuwa Iran ina silaha zake yenyewe zenye uwezo wa kufika mahali popote kuanzia mashariki ya kati, Ulaya na dunia kwa ujumla tena kwa kasi inayoshinda sauti. Watu wakafikiri utani. Sasa kipigo alichotoa juzi ndo kimedhihirisha hilo. Alifyatua mitambo ambayo imesafiri Kilometres zaidi ya 2000 kwa dakika 8 tu, wakati treni ya umeme Dar to Moro inatumia zaidi ya saa 1 na nusu kwa kilometres zisizofika hata 200.
So Netanyahu bado ana muda wa kufanya hivyo mapema, before haujawa too late. Asitegemee sana wazungu ambao wakizidiwa huwa wanakimbia na kuacha kila kitu. Mfano ni hapo Afghanistan. Akishupaza shingo kuna siku atakumbana na mfululizo wa makombora kiasi ya kwamba atashindwa hata kuifikia ndege yake ili apate chance ya kukimbilia Marekani au UK.
Baba wa taifa mwl Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa mtu akishaonja nyama ya mtu basi kuiacha huwa ni ngumu sana. Akimaanisha kuwa mtu huyo ataendelea tu kula nyama ya mtu kama sio dhahiri basi hata kwa kujificha. Hivyo kwa vile Iran ishatest mitambo na kuona kuwa Iron Dome yote ya Israel inavuja, basi hatoacha kuijambisha jambisha ili kuilemaza mifumo ya ulinzi hadi siku dunia itaposhangazwa na tukio ambalo halikufikiriwa kutokea. If you can't beat them just join them ili uwe salama.
Benjamin Netanyahu maji ya shingo, kakutana na mkorofi mwenzake Ayatullah. Yani kama Netanyahu ni kichaa basi Khamenei ni mwendawazimu kabisa. Akisema tutaipiga Israeli basi ujue wataipiga kweli, hata aende sheikh, ustaz, mchungaji au papa kumbembeleza ili asipige yeye atapiga tu, na mzigo utafika vizuri tu kule ulipoagizwa bila kukosea timing au target, kisha Israel na media zao wawe na kazi ya kukanusha na kuficha ukweli wa kipigo.